Beki wa Yanga Hassan Kessy Kuburuzwa Mahakamani na Simba SC!

papason

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Posts
5,119
Reaction score
5,698
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa katika mojawapo ya mechi zilizopita baina ya Simba na Mtibwa Sugar

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwa jazba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.

Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mahakamani kutoa ushahidi wa kile alicho-kisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.

“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.

Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.

“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.

Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.

Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.

Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.
 
Hapo Manara anaposema Yanga ipokonywe pointi tatu sijamuelewa sababu hao hao TFF ndio walioidhinisha Kessy kuchezea Yanga na mambo mengine watamalizana wenyewe
 
Mbona Manara anafoka badala ya kupeleka shitaka mahakamani,mbona ni kawaida kwa Simba kutumia wachezaji kushawishi kuwapa rushwa au amesahau sakata la Ulimb..,tusubiri tuone mwisho wa sinema hii au anataka kusaulisha suala la Boss wake?
 
Wamatopeni wananikumbusha Hayati Mtikila (Mungu amuweke mahali pema peponi). Sasa fasheni yao ni kufungua kesi kwa mwendokasi. TFF wana mashauri sita. Sasa wanataka kwenda mahakamani kwenye suala la Kessy. Waende tu kortini. Wakishinda, Kessy atawalipa kidogo kidogo hadi hizo billion moja zitimie. Teh teh teh
 
huyu manara kumbe sio mweupe mwili tu hadi ubongo wake ni mweupe sana,yaani kutoa droo tu wamechanganyikiwa,anadhani yanga tunatishwa na upuuzi wake?
 
Umetoa hoaj ya kitoto sana. Badala ya kuanisha 'pumba' zake, wewe unashambulia rangi yake? Kutoa droo kuna uhusiano gani na hoja ya Kessy ambayo imeanza kusikilizwa na kamati hata kabla ya ligi kuanza? Jifunzeni kuwa mnajadili arguments za mtu badala ya kushambulia ubanadamu wao
 
Manara nae anajisikia raha kumualibia Kijana anapigana kuhudumia familia yake,yeye atapata faida gani labda?

Niliwahi kutoa angalizo kuhusiana na issu ya Kessy kutokumalizwa kwa ukamilifu na Kamati ya TFF, watu wakaipuuzia.
Nilitoa onyo kuwa kwa kuacha kiporo hili jambo litakuja kusumbua sana, naona sasa ngoma ndio inaanza kwa mbali lkn naamini itasumbua sana. Ni vizuri TFF kutibu magonjwa mapema kdri iwezekanavyo badala ya kuahirisha ahirisha kila mara.
 
Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado.
Nadhani Simba wangeweka mkazo katika kujenga zaidi timu yao na sio hizi frictions, Yanga wapokwe pointi kwa kumchezesha mchezaji ambaye TFF ilimuidhinisha?
 
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa katika mojawapo ya mechi zilizopita baina ya Simba na Mtibwa Sugar

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwa jazba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.

Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mahakamani kutoa ushahidi wa kile alicho-kisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.

“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.

Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.

“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.

Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.

Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.

Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.
Hovyoooo
 
Niliwahi kutoa angalizo kuhusiana na issu ya Kessy kutokumalizwa kwa ukamilifu na Kamati ya TFF, watu wakaipuuzia.
Nilitoa onyo kuwa kwa kuacha kiporo hili jambo litakuja kusumbua sana, naona sasa ngoma ndio inaanza kwa mbali lkn naamini itasumbua sana. Ni vizuri TFF kutibu magonjwa mapema kdri iwezekanavyo badala ya kuahirisha ahirisha kila mara.
Wee unaona sawa mtu kama Kessy kudaiwa hadi bilioni moja au milioni mia hadi mia 2?
Mana kuna hoja zingine hata ukipeleka mahakamani wanaangalia na status na income ya mshtakiwa ili wajidhihirishe vilevile mkataba wa simba hauna kasoro zozote isije kuwa kama ya kina Singano na Kaseja kuambiwa alipe milioni 200 na Yanga mpaka leo kimya ila kesi zao ziliyapa faida magazeti mengi ya michezo
 
viongozi wa simba walitakiwa wamfungulie kessy shauri katika mahakama ya michezo, Kessy alifanya makosa lakini sio kessy peke yake hata Yanga na TFF pia walifanya makosa na hii yote inasababishwa na ubabaishaji wa Tff na Yanga ambao kwa muda mrfu wamekuwa wakivunja sheria na kanuni za michezo.Yanga kwa kujua wamefanya makosa hawakuthubutu kumchezesha kwenye michuano ya Caf baada ya kuonywa ila kwa sababu wanajua Tff huwa hawafanyi kitu juu yao wameamua kumchezesha kweny michuano ya ligi kuu
 
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa katika mojawapo ya mechi zilizopita baina ya Simba na Mtibwa Sugar

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwa jazba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.

Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mahakamani kutoa ushahidi wa kile alicho-kisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.

“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.

Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.

“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.

Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.

Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.

Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.
SAKATA HILI LINANIKUMBUSHA MSEMO USEMAO 'KAMA WEWE UNASEMA WA NINI?? WENZAKO WANAWAZA NITAMPATA LINI HUYO yaliyobakia ni utoto tu
 
Umetoa hoaj ya kitoto sana. Badala ya kuanisha 'pumba' zake, wewe unashambulia rangi yake? Kutoa droo kuna uhusiano gani na hoja ya Kessy ambayo imeanza kusikilizwa na kamati hata kabla ya ligi kuanza? Jifunzeni kuwa mnajadili arguments za mtu badala ya kushambulia ubanadamu wao
akili yako haina uwezo wa kupambanua mambo usidhani ishu ya kesi iko kama unavyofikiria,manara na wenzake ndo wana mambo ya kitoto,haya mambo yameeanza kitambo sio kwa kesi tu,hizo ni figisu za mikia.
 
Umetoa hoaj ya kitoto sana. Badala ya kuanisha 'pumba' zake, wewe unashambulia rangi yake? Kutoa droo kuna uhusiano gani na hoja ya Kessy ambayo imeanza kusikilizwa na kamati hata kabla ya ligi kuanza? Jifunzeni kuwa mnajadili arguments za mtu badala ya kushambulia ubanadamu wao
Wewe nawe umekurupuka sasa,hoja ya kessy ambayo inahusu usajiri na kudaiwa na simba haina uhusiano na swala la rushwa.Hii ni hoja mpya ndugu yetuu.Hii hoja inahusu madai kwamba Kessy katika mahojiano alisema,alipokuwa Mtibwa simba waliwahi kumfuata na kumpa pesa ili aifungishe mtibwa,na akasema ushahidi anao.
 
Lakini 'football' siyo vita na uhasama, haya mambo ya 'kukomeshana' na 'kushikishana adabu' sijui yanatoka wapi? na ndiyo maana soccer letu haliendi mbele!
 
Manara huyu huyuuu,mbona baba zake wana akili sanaaa! Au mama yetuuuuuuu........ndi ndi ndiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom