papason
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 5,119
- 5,698
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa katika mojawapo ya mechi zilizopita baina ya Simba na Mtibwa Sugar
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwa jazba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.
Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mahakamani kutoa ushahidi wa kile alicho-kisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.
“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.
Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.
“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.
Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.
Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.
Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.