Bella: Magufuli ameniambia ananikubali mpaka basi

Bella: Magufuli ameniambia ananikubali mpaka basi

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
xbella.jpg.pagespeed.ic.8k5sLLdX0W.jpg

Christian Bella ameungana na Mrisho Mpoto kwenye orodha ya wasanii waliopo kwenye playlist ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Beatz cha Star TV, Bella alisema Rais Magufuli anamkubali hadi basi! Amesema kwake kukubalika na Rais wa nchi ni heshima kubwa na kumbukumbu atakayoitunza milele.

Bella amedai ni muhimu kwakuwa hajawahi kuwambia kitu kama hicho na rais yeyote tangu aanze kufanya muziki. “Ni kitu kikubwa sana kwangu na sikutegemea,” alisema.

“Sijawahi kuambiwa na na rais yeyote, rais wangu ni Magufuli nampenda sana,” alisema Bella.

Hivi karibuni Mrisho Mpoto naye alionesha furaha yake baada ya Dkt Magufuli kumwambia kuwa anaupenda wimbo wake ‘Sizonje.’
Chanzo: bongo 5
 
Tuache siasa Bella ni Jembe
Sio Rais peke yake
Jamaa anagusa hisia za wengi
 
Hivi huyo jamaa si ni mkongo? Maana amesema eti "….rais wangu ". Yaani sasa hivi anajipachika utanzania!!!!
 
Makubwa tena haya! Kusifiwa, Kusifiwa, Kusifiwa, hahaahah sifa za...
 
Mimi namkubali Bella toka ametoka na kibao cha yako Wapi Mapenzi kiukweli Bella ni the King vocalist melody cc: Nifah, W. J. Malecela
 
Anajipachika uraia Tz mwambieni ajitahidi kulipa kodi mkuu wa nchi hatabiriki
 
mimi bela amenichosha sasa hivi..
apunguze kulia lia kwenye nyimbo zake..
tupate ladha mpya
 
Back
Top Bottom