Belle 9 haamini kama collabo zinaweza kumtoa kimataifa

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Belle 9 amedai kuwa kwenye muziki wake haamini kama collabo ni njia sahihi ya kumfikisha kimataifa zaidi. Akizungumza na Bongo5, Belle amesema wapo wasanii kadhaa walioweza kutoboa bila hata kufanya collabo na wasanii wa mataifa ya nje.

Akizungumza na Bongo5, Belle amesema wapo wasanii kadhaa walioweza kutoboa bila hata kufanya collabo na wasanii wa mataifa ya nje.

"Mimi nimefanya collabo na Joh Makini, I am proud kwa sababu ni msanii mkubwa ambaye anafanya vizuri ndani na nje. Joh is too expensive sio simple tu kufanya naye collabo," amesema Belle.

"Kama unavyojua msanii mkali hawezi kurekodi na msanii mbovu, mimi naamini inawezekana. Mimi naamini collabo sio kitu kinaweze ka kunifikisha International, sijui wasanii wenzangu wengine. Kwa sababu mtu kama Gsan alishiriki mpaka cipher ya BET najua sio kawaida, sasa Gsan alifanya collabo na nani? Na ni washkaji ambao walikuwa level kubwa. Mimi siamini collabo inaweza kunifikisha huko, yaani siamini katika collabo kwa sababu ningekuwa nimeshafanya na nimesharelease. Lakini najua collabo ni maisha ya muziki ambayo inatokea ukafanya lakini mimi sijafikiria nijaribu kufanya ndio nifike huko," aliongeza muimbaji huyo.

Belle anajiandaa kuachia video ya wimbo wake ‘Shauri Zao' iliyoongozwa na Hanscana.

Chanzo: Bongo5

 
Aige wenzake collabo ndo habari mjini hebu ajiulize kwanin msanii mkubwa kama Davido juzi kalilia kufanya collabo na mfalme Kiba, collabo ndo habari mjini.
 
Kwani kuna mpumbavu aliyemfuata akamwambia afanye collabo au ni yeye tu anashoboka na mlinzi wa wanyawa anayesema "eti anaombwa na Davido afanye nae collabo "
 
dogo anajua saanaa sema hana skendo atasubiri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…