Ben Kiko yu wapi jamani?

Watangazaji wa sasa hata hawana mvuto kama huyu jamaa!

kwani sasa hivi kuna mtangazaji. mtu hawezi kutofautisha "R" and "L" lakini anatangaza. Zamani RTD upuuzi huu haukuwepo, qualification ya kwanza ni sauti yako halafu matamshi ya kiswahili fasha.. sio unapenda kutangaza lakini sauti linakwaruza kama chura. Mnawakumbuka akina Jacob Tesha, David Wakati, wakitangaza taarifa ya habari, hata kama hakuna la maana utasikiliza tu zile sauti. Akina Enock Ngombale akitangaza kipindi cha salam, utapenda, akina Abisai Steven, Julius Nyaisanga, Halima Kihemba, sauti zilitulia, na wengine wengi. Sasa hivi hata kama kuna la maana linatangazwa, ile sauti tu inakufanya hata hamu ya kusikiliza huna, mtu ana accent ya kichaga au kisukuma eti ni mtangazaji. Upuuzi mtupu!
 
Ameshatangulia mbele ya haki
 
Benjamin Kikoroma apumzike pema peponi huko aliko. Alikuwa na talent sana katika kipindi ambacho talents zilikuwa hazilipi kabisa.
 
Julius Nyaisanga "Club raha leo Show"ndio namkumbuka maana toka mtoto nilikuwa sikosi kusikiliza zile show.
Na badae tukawa chama la wagonga nyagi,Gin,fegi kino.
Salama mfamao zamani sana pale migo.
Yule mrembo Tumaini Meshack ITV sijui yuko wapi.
Ben Kiko mnyiramba huyu ye ni kikongwe sasa km si marehemu.
 
Rip
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…