Moniel
JF-Expert Member
- Nov 17, 2020
- 274
- 603
BEN MTOBWA..Pengine ni mwandishi bora zaidi wa vitabu vya kiswahili aliyewahi kuishi...
.........."Kwanini umefanya hivyo, Joram?" Nuru aliendelea kufoka.
Joram, ambaye alionekana kimawazo yuko maili kadha wa kadha nje ya chumba hicho, alimtazama Nuru kwa muda. Kisha ikawa kama amemkumbuka. Tabasamu dogo likamtoka, likifuatwa na sauti nzito, "Ilikuwa lazima nifanye vile, iko siku utaelewa Nuru."
"Nitaelewa!" Nuru alifoka, "Nitaelewa nini, mwanamume mwenye heshima zake na hadhi yake duniani anapothubutu kuingia benki na kuiba pesa ambazo nchi na watu wake wote wanazitegemea? Siwezi kuelewa kabisa, Joram. Ambacho naweza kuelewa ni wewe kuondoka sasa hivi na kwenda zako ofisi ya Ubalozi wetu ukaombe radhi na kurudisha kila senti. Tafadhali fanya hivyo, Joram."
Hilo lilisababisha kicheko kwa Joram. "Nina haki ya kula pesa za Tanzania kama wengi wao wanavyozila, Nuru. Huoni watu wenye mishahara ya shilingi elfu mbili wanavyojenga majumba ya mamilioni? Unadhani wanazipata wapi bila ya wizi? Tofauti yangu na wao ni kwamba mimi nimeiba kimachomacho, wao wanaiba kisirisiri. Mwizi ni mwizi tu."
Akasita kidogo kabla ya kuendelea, "Acha tuzitumie Nuru. Acha tuzifaidi. Hii ni nafasi pekee katika maisha yetu ambayo hatujaisahau. Jisikie starehe..."
"Siamini kama maneno hayo yanatamkwa na Joram Kiango. Kwanini umebadilika kiasi hicho Joram?"
Kabla Nuru hajapata jibu mlango uligongwa na kufunguka taratibu. James aliingia. Uso wake ulionyesha kuwa alikuwa na habari ambayo si nzuri sana. Baada ya kubadilishana salamu za kawaida aliwataka radhi na kumchukua Joram chemba.
"Kaka, samahani. Unajua pamoja na kujiita kwako Charles Morris, ni watu wachache sana ambao waliamini? Sura yako si ngeni kabisa hapa Kenya. Umetokea mara nyingi katika magazeti na televishani. Wewe ni yule mpelelezi mashuhuri Joram Kiango. Sivyo, kaka?"
Joram alipochelewa kumjibu, James aliendelea, "Ziko habari mbaya zilizotokea katika vyombo vya habari.
Inasemekana umetoroka kwenu ukiwa umechukua fedha nyingi za kigeni. Kwa jinsi ninavyokufahamu nashindwa kuamini kama ni kweli. Lakini hilo si muhimu sana kwa sasa. Nilichofuata ni kukufahamisha kwamba sasa hivi wapelelezi wa hoteli hii wamekaa kikao wakilijadili suala lako. Waweza kutiwa msukosuko mkubwa. Kwa hiyo, nakushauri utafute mbinu yoyote ambayo itakufanya uokoe maisha yako. Nina ndugu yangu anayeishi Nyeri. Anaweza kukuficha kwa muda."
Joram alicheka na kumshukuru James. "Usijali rafiki yangu. Nitajua la kufanya. Kwa sasa niache nijipumzishe kidogo na kufikiria la kufanya." Baada ya hayo aliutia mkono wake mfukoni na kuutoa ukiwa umeshikilia noti kumi za mia mia ambazo zilidakwa na James kabla hazijamfikia. "Kajipatie bia mbili," alimwambia akigeuka na kurudi chumbani.
"Unaona Joram? Twende zetu ofisi ya Ubalozi," Nuru alimdaka juujuu kwa maneno hayo. "Kufanya nini?" Joram alizungumza kwa upole kama kawaida yake. "Tutakwenda zetu tunakotaka. Sasa hivi uwe binti mtulivu na ufanye kama nitakavyokuambia, tafadhali. Baada ya dakika chache tutakuwa zetu angani tukielekea katika mji mwingine wenye starehe kuliko huu."
"Haiwezekani, Joram. Lazima ukaombe radhi na kurudisha pesa za watu," Nuru aliendelea kukanusha.
"Alikuwa ameishi na Joram kwa muda mrefu. Lakini alikuwa hajapata kumuona Joram anavyokasirika. Leo hii aliziona hasira zake. Aliiona nuru kali na tena baridi, ikijitokeza katika sauti yake ndogo, nzito, aliposema taratibu,
"Haya. Nenda zako ofisi za Ubalozi. Chukua na pesa zetu uwapelekee."....😀😀😀😀😀😀
Unakumbuka vitabu gani vingine vya huyu mwamba wa riwaya?