Ben Paul & Belle 9 amkeni usingizini

Joined
Jun 30, 2015
Posts
38
Reaction score
14
Toka wimbo wa NIKIKUPATA mpaka SOPHIA. Ben Paul ameendelea kuthibitisha ubora wa kipaji chake maridhawa. Belle 9 ni kipaji kingine adhimu katika ardhi ya nchi yetu. Wasanii hawa wawili mpaka leo hawapati thamani na hadhi zao sahihi.

Napenda kuwaamsha usingizi kuwa wanatakiwa kuwekeza katika kazi zao ili watoke kimataifa. Katika dunia ya sasa hivi ili ufanikiwe unahitaji kuwa na kipaji na management nzuri, vijana hawa ni kama wameridhika hivi, lakini ukweli ni kuwa lazima waamke ili kufika juu zaidi.

Nakaribisha hoja zaidi..
 
Hizi team ziuwawe kwanza tofauti na hapo hamna kitu! mfumo mbaya wa uongozi kujituma hawataki basi watoe wimbo halafu sisipigwe tujue tatizo media! wimbo wa sofia ume hit lakin yupo kimya
 
Kama Huyu belle 9 sijui Hana washauri au vipi. Dogo anajua sana ila naona kama hajitambui kabisaa.
 
Hizi team ziuwawe kwanza tofauti na hapo hamna kitu! mfumo mbaya wa uongozi kujituma hawataki basi watoe wimbo halafu sisipigwe tujue tatizo media! wimbo wa sofia ume hit lakin yupo kimya

Ben pal & belle9 walianza kuimba lini?

Team zimezaliwa mwaka gani ?

Haiwezekani wote kua bill gate
 
Hawa jamaa tatizo lao ni marketing mbovu

Kuimba is the tip of the iceberg,inabidi wajitangaze vya kutosha
 
bora ben paul anajitahidi kwa mbali ila belle 9 kazubaa sana, akina baraka da prince wanatake over hao wapo tu
 
Wasisingizie team, wajipe upya kuhusu management zao, Jux mwenzao naona kaamka hiv karbun tutaanza kumuona kwenye international Awards,

Belle9 ajipe upya hasa campan inayomzunguka muda wote anashinda na wasanii wa hip pop wakina stamina nyandu toz young killer sijui watamfikisha wapi. Campan yake ilitakiwa wawe wakina Mondy, kiba, Navy kenzo, vanesa mdee ili wampe maujanja ya kutoboa kimataifa.

Kuhusu Ben pol at least ameanza kupaa maana hata kwenye coke studio mwaka huu kaingia hope ataitumia hiyo exposure vizuri, mfano ule wimbo wa Sophia alitakiwa afanye remix hata na msanii yeyote mkali wa nje ya nchi angeweza kufika mahali pazuri.

Siri ya mafanikio ni kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, wasilalamikie team kwani hata hao wakna Kiba na Mondy hizo team walizipata baada ya kuonyesha juhud hivyo hata hao wakina Belle n Ben paul wanao uwezo wa kuunda team endapo watabadilika.
 
Belee9 ametengwa na washikadau wa soko la muziki Tz baada ya kuzinguana, Ben Pol ashindwe mwenyewe tu

Nchi hii kuna washenzi wachache wamekamata kila engo ya muziki yaani ukipishana nao tu unawakati umgumu sana kuendelea

Jide anapambana na mfumo huo lakini sasa ni kama ameisha jikatia tamaa
 
Wapo na wataendelea kuepo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…