Ben Pol: Nilichokilenga kimefanikiwa

GTA

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
878
Reaction score
651
Leo kwenye Jahazi la Clouds fm Benpol amefunguka na kudai kuwa kile ambacho alikilenga katika kupiga picha hizo kimefanikiwa kwa asilimia 100%.

Benpol amefunguka kuwa picha zile zina maudhui kulingana na wimbo wake anaotarajia kuutoa masaa machache yanayokuja, kulingana na kazi yake ijayo inahusisha mambo ya utekwaji ndio maana aliamua kufanya kitu kama hicho.
 
Ben Pol aliporelease picha zile watu mapovu yaliwatoka sana. Hawakutaka hata kufuatilia sababu ya ben pol kupiga picha zile. Nakumbuka nilikuwa nasema tena kwa msisitizo kuwa Ben pol si mwehu kivile, ana maana yake, pengine anatengeneza video. Sasa leo sijui watasemaje.
Nchi za wenzetu kwenye wasanii waliopiga hatua vitu kama hivi vipo kila siku. Tanzania msanii akifanya ni inshu. ifikea hatua wabongo -ofcourse na wakenya na waganda tubadilike
 
Kwa hiyo msanii akitaka kurelease wimbo unaohusiana na kutekwa inabidi apige picha tako nje?
Nchi za wenzetu nchi za wenzetu kwani lazima tufanye kama wao mbona wenzetu wahindi wanajitahidi kufanya yao na wametusua mpaka hollywood wanawaelewa.
Ukimuuliza atakwambia sijui mbona flani wa narekani alifanya hivi... Sisi siyo wamarekani.
 
ulitaka apige akiwa kavaa kanzu wakati scene haihitaji kanzu? Kabla hujahukumu kitu tafuta kwanza maudhui ya hiyo kitu, ufanye upembuzi ndio utoe hukumu. kwa kifupi mnaolaumu na kulalama mlikurupuka tu
 
Wale wana maadili yao na tamaduni zao.. ambazonni tofauti na za kwetu.
Kwao wakifanya powa.. ila kwetu lazima tuone ni kitu cha ajabu.. why? Sababu si tamaduni zetu mtoto wa kiume kupiga picha kama ile
 
Haya bwana Detective J , sasa tuzungumzie tamaduni zetu, bila shaka ni za kibongo. Kwenye tamaduni zetu kuna kibaya kipi fanani kutengeneza kazi yake ya sanaa na kuonesha matukio halisia kulingana na maudhui yake?
 
ucha kuwa mtumwa wa fikra ndugu unaposema kwenye nchi za wenzenu hv vtu ni vya kawaida hii ni tanzani jifunze kusimamia tamaduni na taratibu za taifa lako kwanin uishi maisha ya jirani yko wakati wewe unamisha yko mambo ya kuiga yanatupoteza ndo mana hata muziki wetu unakosa soko la kimataifa coz tunashindia kukopy na kupest hebu tuachane na utumwa tuwe wabunifu kma wimbo ni mzuri utapendwa tu na kama ni mbaya hautapendwa kamwe hta kama angepiga picha akiwa na mkewe kitandani wana.....x
 
ulitaka apige akiwa kavaa kanzu wakati scene haihitaji kanzu? Kabla hujahukumu kitu tafuta kwanza maudhui ya hiyo kitu, ufanye upembuzi ndio utoe hukumu. kwa kifupi mnaolaumu na kulalama mlikurupuka tu
Kwa hiyo mtu akitaka toa ngoma ya mapenzi apige akiwa uchi kitandabi na mpenzi?
Ndicho unachojaribu kusema?
Ukweli ni kwamba kupiga picha makalio nje mtoto wa kiume hakufai kuungwa mkono na wanaume sisi siyo wa marekani hatujafika huko na sidhani kama inafaa tufike huko.
 
mbona nyimbo zote alizoimba hakupiga picha yoyote na zilikubalika iweje hii..tatizo wasanii wetu wanaishi kwa kiki ubunifu ziro
 
umeongea point ndugu yani kama hata benpol amefikia huko mtu ambaye ndo alikuwa katika kundi la wchache wenye mfano bora kwa jamii amefanya hvyo daah inasikitisha sn
 
Ben Pol ni msanii mzuri. Kaifanyia haki kazi yake ya sanaa. Utamaduni ni pamoja na ubunifu. Sasa mlitaka tanzania tuendelee kuishi ma mavazi ya ngozi za wanyama na kaniki kwa vile tu ni utamaduni?
 
umeongea point ndugu yani kama hata benpol amefikia huko mtu ambaye ndo alikuwa katika kundi la wchache wenye mfano bora kwa jamii amefanya hvyo daah inasikitisha sn
Yani sasa hivi wasanii wamehama kwenye kuamini katika kutoa mziki mzuri wameamia kwenye kuamini kuwa kik ndo zinasukuma mziki.
Nashangaa kuona mwanaume anaunga mkono ujinga huu.
 
Ben Pol ni msanii mzuri. Kaifanyia haki kazi yake ya sanaa. Utamaduni ni pamoja na ubunifu. Sasa mlitaka tanzania tuendelee kuishi ma mavazi ya ngozi za wanyama na kaniki kwa vile tu ni utamaduni?
Hivi unasoma unachokiandika.
So mtu akitaka kuimba kuhusu mabaya ya ushoga atengeneze posta ya mwanaume akibanjuliwa then aiweke mtandaoni?
 
Kwa hiyo ukitekwa unavuliwa nguo,unafungwa mikono alafu unapakwa mafuta kuanzia mgongoni mpaka kwenye makalio alafu wanakupiga na picha au sio?!

Kama ujumbe ulikuwa kutekwa kwanini akutekwa akiwa na nguo zake kulikuwa na ulazima gani wa kutuonyesha makalio yake yenye mafuta?!
 
Hivi unasoma unachokiandika.
So mtu akitaka kuimba kuhusu mabaya ya ushoga atengeneze posta ya mwanaume akibanjuliwa then aiweke mtandaoni?
Acha kuongeza chuvmvi. Kuna ubauya upi mtu akiigiza akiwa hajavaa nguo? Acheni fikra finyu. Mwenzenu ben pol sasa anatengeneza pesa kwa picha alizopiga. aliijua hadhira yake na ndiyo inayomwingizia pesa. nyie endeleeeni kupiga kelele eti yuko uchi yuko uchi....
 
Ben kafanya upuuzi na ukimtetea mpuuzi na wewe lazima tukuone mpuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…