Benchi la ufundi Simba liambiwe ukweli, Saido Ntibazonkiza siyo mchezaji wa dakika 70

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Najua kocha anapenda kumtumia Saidoo ntibazonkiza kwa sababu ya profile yake lakini ukija kwenye pitch huyu Saidoo hakupi unachotaka.

Kuna mchezaji Kama Miqson, kibu denis Hawa wanafaa kupewa dakika nyingi za kucheza kuliko Saidoo ntibazonkiza anayekua Bora kwa dakika 30 akizidisha hapo anatepeta kabisa anakua ni mchezaji wa kupoteza mipira.

Mchezo dhidi ya Al ahly Saidoo hakustahili kucheza dakika 70, ilibidi atoke mapema iingie nguvu mpya nguvu Kasi ambapo pengine tungezungumza mengine kutokana na mipira aliyoipoteza Saidoo na golden chance zingezaa matunda.

Maoni Yangu: Saidoo ntibazonkiza Umri umeenda dakika 30 zinamtosha tofauti na hapo anakua mzigo benchi la ufundi liangalie kwa jicho la tatu nani anaweza kufit nafasi anayocheza Saidoo ntibazonkiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…