Benchi la ufundi Simba

Brazil ya 98 na 2006 ilikuwa na vikosi bora lakini haikubeba kombe sababu makocha wao walikosa mbinu za ziada
Kuna ile Liverpool ilikuwa Kali ikapata points 94 lakini Ubingwa alichukua City, kutokuchukua Ubingwa hakuondoi uwezo wa Kocha, 1998 Brazil si alifungwa fainali na Ufaransa??Unalaumu kocha pia.Anyway Mimi hoja Yangu haiko huko, Hoja Yangu kuu ni kwamba, sio dhambi team kunyanyuliwa na individual performances na hilo sio kiashiria kuwa Kocha ni Mbovu.Alete hoja nyingine za kuelezea Ubovu wa Kocha na sio kusema team inabebwa na Uwezo wa Wachezaji binafsi.Hilo ni kawaida tena kwenye soka la ngazi ya juu zaidi
 
Brazil ya 98 na 2006 ilikuwa na vikosi bora lakini haikubeba kombe sababu makocha wao walikosa mbinu za ziada
Wataalam Wa soka wanasema hizo ndio nyakati za Mwisho za Soka la Brazil kuanguka kwa kutegemea Kizazi kinachocheza soka la Kiulaya na Kuachana na Soka la Kibrazil, Leo wabrazil wanaenda ulaya mapema sana wanajikuta wana Akili na Maarifa yote ya kiulaya kinyume na akili za Samba zilizoiweka Brazil kileleni.Na Tangu hapo Brazil imekuwa tia tia maji.Kw sura pana hilo halina uhusiano na makocha
 
Ila watu wanataka kuwa vipofu sababu ya ushindi wa jana. Timu imeshinda sababu ya ubora wa wachezaji lakini mbinu tulikuwa ovyo.
 
Wazee mmeandika kile kipo mawazoni mwangu. Hakuna game plan kabisa. Na Chama kweli hii hulka anayo toka zamani. Anaweza kuua move nzuri iiyokwisha anzishwa
Hope wataleta mtu mwenye cv ya kueleweka hasa kufundisha hadi nusu fainali champion league
 
Ongeza milovan cirkovic Sina uhakika na spelling bt alitoka serbia alikuwa bonge la kocha japo hakudumu
Umenikumbusha mkuu, tatizo letu Simba vitu vizuri hatuvikumbatii.....enzi za Siang'a sukuona sababu ya kumwachia aondoke kwenda zake. Simba ilikuwa Simba kweli enzi zile.....

Amekuja uchebe Simba ikawa mwamba kweli kweli...kuwafunga Waarabu sio kitoto...niliumia mnoo kuondoka kwa kocha yule.
 
Unamaanisha Patrick Phiri Mzambia? Au James Sianga Ojwan'g maana awa ni watu wawili tofauti na wamefunfisha Simba kwa muda tofauti, hebu tufafanulie nahisi umetuchanganyia madesa mkuu.
Ngoja ni-edit
 
Ngoja ni-edit
Asante kwa kuelewa, yule James Sianga Ojwan'g alikuwa mwamba kweli, aliwaondosha waarabu na figusu zao Kyle kwao Egypt, japo inasikitisha aliondoka Simba sc kwa kudharauliwa kibaya zaidi alikufa akiwa anawadai Simba sc malimbikizo ya fedha zake za mishahara mzee wa watu.
 
Na huwa nikifika hapo tu nachoka na soka letu. Tukipata makocha wazuri tunawafukuza kama maharamia. Tukipata wasiofaa tena tunaanza kulaumu tu.

Ifikie wakati viongozi wa timu zetu wajue sisi mashabiki huwa tunataka soka la kiwango na ushindi toka kwa timu zetu. Hata timu inashinda kama haioneshi soka pira biliani sisi haturidhiki kabisa.

Watu wanapenda EPL sababu kule ndiyo kitovu cha pira biliani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…