Bendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni ruksa kuibadili?

Bendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni ruksa kuibadili?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Jana Jumamosi 15/04/2023 Waziri Mkuu alikuwa Zanzibar akizindua kitabu cha taarifa ya Sensa iliyopita, kwenye uzinduzi huo walikuwepo wananchi ukumbini ambao walikuwa wakipepea bendera za taifa, kitu ambacho sikuelewa ni hizo bendera za taifa katikati kuwa na picha ya rais mama Samia!

Bendera yetu ya taifa ipo kikatiba na inalindwa na sheria ambayo hairuhusu mtu yeyote kubadili sehemu yoyote ya bendera hiyo, sasa ni vipi hii imebadilishwa na ni kwa idhini ya nani? Ni vizuri serikali itufahamishe kuhusu uwepo hiyo picha kwenye bendera ya taifa.
 
Jana Jumamosi 15/04/2023 Waziri Mkuu alikuwa Zanzibar akizindua kitabu cha taarifa ya Sensa iliyopita, kwenye uzinduzi huo walikuwepo wananchi ukumbini ambao walikuwa wakipepea bendera za taifa, kitu ambacho sikuelewa ni hizo bendera za taifa katikati kuwa na picha ya rais mama Samia! Bendera yetu ya taifa ipo kikatiba na inalindwa na sheria ambayo hairuhusu mtu yeyote kubadili sehemu yoyote ya bendera hiyo, sasa ni vipi hii imebadilishwa na ni kwa idhini ya nani? Ni vizuri serikali itufahamishe kuhusu uwepo hiyo picha kwenye bendera ya taifa.
Maumivu ni pale utakapoambiwa bajeti ya kuzichapisha
 
Maumivu ni pale utakapoambiwa bajeti ya kuzichapisha
Hapana, bendera ya taifa inalindwa na katiba na sheria na mojawapo ni pale inaposhushwa iwapo upo kwenye eneo hutakiwa kusimama, ukikutwa umeikanyaga au unaichoma moto utaona cha mtemakuni. Sheria inasema wazi kuhusu rangi 4 na upana wa miraba, pia hairuhusu nyongeza yoyote kwenye hizo rangi na bendera yenyewe.
 
Hicho ulichokiona ni bendera au kitambaa chenye bendera na picha ya Mama?
 
Unataka kusema nini?

Nnatakakupata maelezo kuhusu kinachoitwa bandera ya taifa iliyobadilishwa.

Tusipokua makini ipo siku mtu utavaa nguo zenye rangi zilizopo kwenye bendera utaambiwa umebadili bendera. Kuna leso Zina rangi za bendera ya taifa, Sasa hapo nimeulizwa ukute vipeperushi maalum au vitambaa vimetengenezwa Kwa rangi za bendera yetu na kupambwa Kwa picha ya Mama Kisha mtu anasema bendera imebadilishwa.
 
Nikichukua kitambaa nikakipaka rangi za Taifa halafu nikaweka picha yangu katikati inaruhusiwa?
 
Nikichukua kitambaa nikakipaka rangi za Taifa halafu nikaweka picha yangu katikati inaruhusiwa?

Weka picha ya kinachoongelewa kwenye hoja ndio maana nimeuliza tunajadili bendera ipi?
 
Back
Top Bottom