Bendera ya Marekani kupepea nusu mlingoti kwa siku 3 kuomboleza waliokufa kwa Corona

Bendera ya Marekani kupepea nusu mlingoti kwa siku 3 kuomboleza waliokufa kwa Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
0dc6d1a1fda77291bfb229f49191b20d

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri ya bendera ya nchi hiyo kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, kuomboleza vifo vya Wamarekani waliokufa kutokana na virusi vya corona.
Trump ameamrisha hatua hiyo, baada ya idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 kukaribia 100,000 nchini humo.

Aidha Trump amesema bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa nchini humo, kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani.

Imeelezwa kuwa Ingawa idadi ya vifo vya kila siku nchini humo haijaongezeka, watu bado wanaendelea kupoteza maisha, na hesabu kamili inapindukia vifo 94,500 ikitajwa kuwa ni taifa lenye vifo vingi ulimwenguni.

Wiki hii Marekani imerikodi vifo 1,300 kwa siku, vinavyotokana na virusi vya corona.
 
Haisaidii kitu,Watu wanakufa wewe unapeperusha Bendera nusu mlingoti,Tafuta dawa hizo hizo ngonjera waachie Malenga.
 
Trump amekwama wap ? bongo kila baada ya hatuta 3 unakuta ndoo ya maji na sabuni. yeye kashindwa kununua hata ndoo aise kuweka mitaan?
 
Naona Chainizi inawatoa jasho

Mungu awasaidie ila yote kayataka yule mpuuzi wa Tramp Mzee kibwengo sana yule

Sent using My COVID-19
 
Kuchelewa kuchukua hatua za udhibiti mapema kumeigharimu Marekani. Pole sana kwao.
 
Asambaze koki za maji na sabuni kila mtaa itasaidia kidogo


Sent using samsung A50
 
Back
Top Bottom