Bendera ya Marekani pekee ndio itakayoruhusiwa kupepea

Bendera ya Marekani pekee ndio itakayoruhusiwa kupepea

Snipes

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2013
Posts
9,165
Reaction score
16,791
Serikali ya Donald Trump imetambulisha sera ya bendera moja, ambapo bendera ya Marekani pekee ndiyo itakayoruhusiwa kupepea katika vituo vyote vya Serikali ndani na nje ya nchi zikiwemo ofisi za balozi.

Bendera nyingine zitakazoruhusiwa kwa maadhimisho ya siku maalumu ni ya mfungwa wa vita na ile ya waliotekwa ama kufungwa kinyume na haki.

Aidha, mfanyakazi yeyote wa serikali atakayekiuka sheria hiyo atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi au kuvunjiwa mkataba wake.

Amri hiyo imesisitiza kuwa bendera ya Marekani ndio bendera pekee inayowaunganisha Wamarekani wote chini ya kanuni za haki, uhuru na demokrasia.

Chini ya serikali ya Joe Biden, bendera kadhaa zilionekana zikipepea katika majengo ya serikali ikiwemo ya kuwakilisha watu wa jinsia mbalimbali na mahusiano ya jinsia moja.

#KitengeUpdates
 
Back
Top Bottom