Bendera ya Zanzibar ikipandishwa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa 10-12-1963.

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA NCHI YA ZANZIBAR.

Maajabu ya serikali na chama cha mapinduzi CCM, ni kawaida kwao kuyatukuza mapinduzi ya Zanzibar na kuupuuza Uhuru wa nchi hiyo, wakijitoa ufahamu kuwa kusingekuwepo na mapinduzi kama nchi hiyo haikupata kuwa huru kwanza, mnamo 12/01/1963.

Pichani, Bendera ya Zanzibar ikipandishwa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa 12-01-1963.

Mapinduzi yaliyoratibiwa mjini Dodoma ndiyo yamekuwa msingi wa kulazimisha utawala wa CCM kujibakiza madarakani kwa nguvu, na niwaibie siri moja ndugu zangu: Chama cha mapinduzi ilipaswa kuwa ni chama cha Zanzibar na sio Tanganyika, maana Tanganyika hakuna mapinduzi tuliyoyafanya na mapinduzi yanayozungumzwa ni mapinduzi ya Zanzibar. Kwa mtanganyika kuimba 'Mapinduziii, daimaaaa' ni zaidi ya wehu.

Naweza kudiriki kusema kuwa Muungano uliopo sasa ni muungano wa vyama na sio wa nchi, muungano wa nchi no ule tulioupendekeza wakati tulipotoa maoni yetu juu ya katiba mpya (rasimu ya warioba), yaani serikali tatu.

Muungano wa sasa umeshikiliwa kwa maslahi ya chama kimoja cha mapinduzi (mapinduzi ya Zanzibar), na sio kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili, yaani Zanzibar na Tanganyika.

Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa nchi ya Zanzibar ni tarehe 12/01/1963.

Happy Birthday Zanzibar..

 
Tunaomba na picha ilivyoshushwa mwaka 1964 baada ya muungano wa zimbabwe na Tanga..... kama alivyosema Mlugo the Don!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…