Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Benedict Daswa alizaliwa mnamo tarehe 16 Juni 1946,huko nchini Afrika ya Kusini,alizaliwa ktk kabila la Wavenda.Utotoni aliitwa Tshimangazbo Samwel Daswa,kabla ya kuwa Mkristo Mkatoliki kwani alizaliwa katika familia ya Kipagani.Hivyo alibatizwa ktk Kanisa Katoliki mnamo tarehe 21 Aprili 1963 akiwa na miaka 17;alichagua jina la Benedict kwa vile alivutiwa na maisha ya Mtakatifu Benedikto wa Nursia na pia akachagua falsafa ya Mt.Benedikto ya "Ora et labora" yaani "Sala na kazi".Alipata Kipaimara tarehe 21 Julai 1963.Mwaka 1980 alimuoa Evelina,Mungu akawajalia watoto nane(8).
Benedict Daswa alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi lakini pia akawa mwalimu wa dini(Katekista).Akiwa mwalimu mkuu unaambiwa aligombana sana na wazazi waliowaachisha shule watoto wao hasa wa kike wasisome shule,alikuwa tayari hata kuwalipia.Aidha alijisikia raha kusaidiana kazi za nyumbani na mkewe(Evelina) kinyume kabisa na Wanaume wengi wa Kiafrika(Wanaume wenzangu tupo hapo?).Benedict Daswa na mkewe walikuwa marafiki na si nyapara na kijakazi wake.Daswa alisaidia wagonjwa,wazee,na wahitaji kwani alijawa upendo si haba.
Benedict Daswa alijitolea kujenga kanisa mtaani ili watu wamwabudu Mungu humo.Huyu ndio Benedict Daswa aliyejawa upendo kwa Mungu na kwa jirani.
BENEDICT DASWA NA VITA DHIDI YA IMANI ZA KISHIRIKINA.
Benedict Daswa alipinga sana Imani za kishirikina,alipiga vita mambo ya kusema eti Fulani ni mchawi,mambo ya kupiga ramli na yote yaliyohusu ushirikina yalipigwa vita na huyu mwanaume kutoka pembe ya kusini mwa Afrika.
Unaambiwa huyu mwamba alianzisha timu ya mpira iliyojulikana km "Mbahe eleven computers" ambayo aliiendesha kwa fedha zake mwenyewe,lkn aliamua kuiacha timu hii pale wazee na kamati ya ufundi waliposema waende kwa Sangoma kusaka dawa ya kuzindika timu ili kushinda kwenye mashindano(Upuuzi unaendelea hadi leo hii hapa bongo).Akaamua kuanzisha timu nyingine ya mpira iliyojulikana km "Mbahe Freedom rebels". Daswa alikuwa pia Katibu wa mikutano ya halmashauri ya kijiji.
Mnamo Novemba 1989 kulitokea mvua kubwa sana iliyoambatana na radi na hali hiyo ikajirudia tena mnamo Januari 1990,ambapo ilisababisha madhara mengi sana pale kijijini,Wazee wakashauri kuwa upitishwe mchango kwa kila mwanakijiji kiasi cha Rand tano(5) za Afrika ya kusini ili waweze kwenda kwa wataalamu(SANGOMA)kujiuliza,kumtafuta mchawi au msababishi wa tatizo hilo.Benedict Daswa alikataa kata kata kutoa mchango huo,Daswa aliwaambia wazee hivi " Hakuna mchawi hapo,radi ni jambo la kimaumbile tu(is just a natural phenomena) ni mgongano wa mawingu yenye umeme ambapo chaji chanya(+) na hasi(-) zinagongana na kusababisha moto,moto huo ndio radi yenyewe ambayo husababisha maafa".Hapa aliwachefua wazee na wale walioamini sana ushirikina hivyo akachukiwa sana.
Siku moja,tarehe 2 February 1990,akiwa anatoka mjini na shemeji yake na mgonjwa na mtu mmoja aliyekuwa ameomba rifti,basi alimshusha shemeji yake nyumbani na akapitiliza kijiji cha mbele kumpeleka aliyeomba rifti,usiku wakati anarudi akakuta njia ile imezibwa na miti iliyokuwa imeangushiwa barabarani,aliposhuka ili kuiondoa miti hiyo basi alivamiwa na kundi kubwa la watu waliompiga sana,akakimbilia kwenye kibanda cha karibu alimokuwa kuwa anaishi mama mmoja ili kunusuru maisha yake lkn wapi,si unajua tena "Siku ya kufa nyani miti yote hutereza!!!!". Basi Yale majamaa yakamfata yakamtishia yule mama mwenye kibanda kuwa yatamuua,Benedict Daswa ikabidi atoke tu nje,akauawa kinyama sana na hao wauaji,kwa ukatili mkubwa alimwagiwa maji ya moto puani na masikioni ili kuhakiki km kweli amekufa.Benedict Daswa mwanaume wa shoka alikufa kishujaa akiitetea Imani yake kwa Mungu,akakata roho akisema" BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU".Huyu ndio Benedict Daswa mwafrka mwenzetu aliyethubutu kupiga vita Imani za kishirikina.
Kanisa Katoliki,kupitia Papa Francisco, Mwaka 2015,lilimtangaza Benedict Daswa kuwa Mwenye heri na Shahidi wa Imani.
Wapendwa wana JF ,najua tupo wa Imani mbalimbali basi kwa wale wa Imani km yangu,Benedict Daswa anatufundiaha kukataa Ushirikina kwa nguvu zote,haijalishi utapata maadui kiasi gani,hata zile mila na desturi zisizofaa tuzipige chini,maana ni upuuzi tu.Tuwaelimishe wenzetu kuwa si kila tatizo ktk jamii limesababishwa na ushirikina,tujikomboe kifikra.
View attachment 1575375
Huyo aliyesimama,mwenye koti na tai ndiye Benedict Daswa