Benin: Watatu, akiwemo Waziri wa Zamani wakamatwa kwa njama za mapinduzi

Benin: Watatu, akiwemo Waziri wa Zamani wakamatwa kwa njama za mapinduzi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Watu Watatu, wakiwemo Waziri wa zamani na Mkuu wa Ulinzi wa Rais Patrice Talon, wamekamatwa kwa tuhuma za kupanga mapinduzi, huku uchunguzi mkali ukiendelea ili kuwabaini Wahusika wengine

Mwendesha Mashtaka wa Serikali aliwaambia Waandishi wa Habari, Waziri wa zamani wa Michezo, Oswald Homeky, alikamatwa Septemba 24, 2024 akimkabidhi Mkuu wa Walinzi wa Rais, Elonm Mario Metonou, Mifuko 6 ya pesa

Wapelelezi walisema Kanali Djimon Dieudonne Tevoedjre alikuwa akihongwa ili asipinge mapinduzi yaliyopangwa kufanyika Septemba 27, 2024 nchini humo

Pia alikamatwa mfanyabiashara, Olivier Boko, rafiki wa Rais Talon, ambaye hivi karibuni alionyesha kuwa na malengo ya kisiasa. Mawakili na wafuasi wa Boko walilaani kukamatwa kwake wakikiita "utekaji nyara" na wanataka aachiliwe mara moja. Uchunguzi unaendelea kubaini washukiwa wengine, mwendesha mashtaka alisema.

Kumekuwa na mapinduzi ya kijeshi mara nane na majaribio kadhaa ya mapinduzi tangu mwaka 2020 katika Afrika Magharibi na Afrika ya Kati, maeneo ambayo yalikuwa yamepiga hatua kuondoa sifa yake kama "ukanda wa mapinduzi," lakini ukosefu wa usalama na ufisadi unaoendelea umefungua tena mlango kwa viongozi wa kijeshi kuchukua hatua
 
Back
Top Bottom