Benjamin Mkapa: Shujaa aliyeona umuhimu wa kuimarisha Serikali za Mitaa

Benjamin Mkapa: Shujaa aliyeona umuhimu wa kuimarisha Serikali za Mitaa

mavumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
596
Reaction score
328
Kwaheri Ben!

Katika mambo ambayo uliyafanya na hatutasahau ni pamoja na kuona umuhimu wa kuziimarisha Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mwaka 1998 Rais Mkapa alianzisha mpango ulioitwa Local Government Reform Program Tanzania.

Mpango huu ulikuja wakati muafaka maana kipindi hicho Halmashauri zilikuwa zimefikia kiwango cha udhaifu ajabu, hata hakuna aliyejua zitaishia wapi.

Mambo yalikuwa ovyo ovyo kwelikweli na hata Madiwani hawakujua wao ni nini, sio wao ni nani, hapana hawakujua wao ni nini!

Mkapa alizinyoosha Halmashauri na hadi sasa hali ilivyo ni kutokana na kazi aliyoifanya Brither Ben Mkapa.

Baada ya hapo hadi vyuoni somo la Local Government limeshika kasi na hakuna Mtanzania asiyeujua, umuhimu wa local government ukiacha wachache wenye husda!

Kwaheri Ben.
 
Kawaida Mtu akishatangulia mbele ya haki hasa kwa utamaduni wetu watu weusi, renzo kama hizi Guinness na kila mnufaika wa kati ya taifa.
 
mavumbi,

Sasahivi halmashauri hazina tofauti na ofisi ya DAS, vyanzo vya mapato yote wamenyang'anywa, watumishi karibu wote idara muhimu zimeondolewa(Babaraba, Maji, Ardhi na maliasili na utalii n.k)
 
KAMA NAFSI ZA WALIOFARIKI HUWA ZINABAKI NA KUENDELEA KUSIKIA YANAYOENDELEA UKU DUNIANI BASI UYU MAREHEMU NDG MKAPA ATAKUWA NA MAUMIVU MAKUBWA YA KUSHINDWA TENA KUJIINGIZA KTK UCHAGUZI HUU UJAO NA KUIBA KURA YANI KUYACHAKACHUA MATOKEO YA KURA ZILIZOPIGWA NA WATANZANIA KWA LENGO LA KUISAIDIA CCM
Banza stone alimaliza hujafa hujasifiwa
 
mavumbi,

Sasahivi halmashauri hazina tofauti na ofisi ya DAS, vyanzo vya mapato yote wamenyang'anywa, watumishi karibu wote idara muhimu zimeondolewa(Babaraba, Maji, Ardhi na maliasili na utalii n.k)
Ni kweli ila baada ya muda watakuja tambua kosa hili la kuzififisha Halmashauri ...mark my words
 
Mkapa aliifanyia hii nchi mambo makubwa, Alijenga mifumo na taasisi Imara
Mkapa alikuwa rais bora
Sawa kabisa nchi hii inakosa MIFUMO na TAASISI imara ndio maana mambo hayaendi na nchi imekuwa ikiongozwa kwa matamko tu. Apumzike kwa amani.
 
Kabisa kabisa. Alihusika na mauaji ya wapemba wasio na hata 2001
Unauhakika??? We we umekalilishwa, unachuma dhambi bure, ..... Kwanza Wakati vifo vinatokea Mkapa alikuwa nje ya nchi anatibiwa.................mbona huwataji waliohitisha maandamano yasiyo na kibali, mbona huzungumzii polisi walio uwawa bila hatia....
 
Mifumo inayotawala nchi kwa sasa, Mkapa alifanya kazi kubwa.

Mkapa alisimika mifumo ifuatayo!

1.TCU
2. NSSF
3. Uwanja wa mpira wa Taifa
4. Ofisi za Umma kuanza kuwa na hadhi
5. Mpango wa Elimu ya msingi MMEM
6. Mpango wa kupunguza umasikini MKUKUTA
7. Mpango wa kurasimisha biashara MKURABITA
8. Wakala wa Barabara TANROADS
9. Kusamehewa Madeni
10. MEMKWA
11. Kupandisha pato la Mtanzania kutoka dola 170 mwaka 1995 hadi dola 500 mwaka 2005 kwa mwaka (Ongezeko la Gross National Income per Capita)
12. TBC
13. Kuboresha huduma za Afya za hospitali za serikali
14. Kuongeza shule za sekondari nchini mifano michache ni kama vile shule ya Kambangwa na Benjamin Mkapa Dar

15. VAT
16. NHIF
17. Daraja la Mkapa la Mto Rufiji
18. Aliacha Hazina iliyonona
19. LOANSBOARD

Mkapa alijenga Taasisi ambazo hadi leo tunanufaika nazo
 
Unauhakika??? We we umekalilishwa, unachuma dhambi bure, ..... Kwanza Wakati vifo vinatokea Mkapa alikuwa nje ya nchi anatibiwa.................mbona huwataji waliohitisha maandamano yasiyo na kibali, mbona huzungumzii polisi walio uwawa bila hatia....i

Utani mwingine bana, yaani uporwe ushindi kisha ukaombe kibali cha kuandamana kwa aliyekupora ushindi? Kwani yeye kuwa nje ya nchi ndio hawezi kutoa amri, au ulidhani hata angekuwepo hapa nchini, yeye ndio angekaa mstari wa mbele?
 
Back
Top Bottom