Benki gani hawana mlolongo kwenye kukopa kwa kutumia hati ya nyumba?

Benki gani hawana mlolongo kwenye kukopa kwa kutumia hati ya nyumba?

Rufaro

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
222
Reaction score
342
Wakuu

Naomba tushirikishane ni benki gani nchini ambayo haina msururu wa mambo mengi katika kukopa kwa kutumia hati ya nyumba.

Asanteni.
 
Sidhani kama zipo maana itabidi
1. Kuhakiki nyaraka uhalali
2. Kuhakiki umiliki jina
3. Kuhakiki eneo kama ni kweli lipo na lina nyumba nk
4. Kufanya tathmini ya thamani
5. Historia ya miamala
6. Biashara unayofanya
7. Mapato yako kwa siku, mwezi
8 . matumizi, baki na faida
9. Kiwango cha mkopo
10. Marejesho
12. Mashahidi no

Hayo mambo popote hayakwepeki

Kwahio hazipo sababu hizo njia hawataziweza kuzifanya au ndio sijaelewa , mana naona hizo njia ulizozitaja nilitegemea au nategemea kwamba ndio kazi ya benki kitengo cha mikopo wanatakiwa kufanya, na mimi kama mteja au mteja mwingine yoyote huwezi kua na hati jina tu au hati karatasi tu ilihali lazima uwe na tangible evidence.
 
USHAUR wangu,

Nenda NMB, ila hakikisha una Biashara iliyosajiliwa na kutambulika serikalini (tra,MANISPAA n.k)

Na umejikamilisha Kama alivyosema hapo juu bwana Mshana Jr

Suala la hati Sikuhizi sio Lazima Sana,
Mashahidi wa pande nne za nyumba yako na viongoz wako wa serikali ya mtaa kuthibitisha kweli nyumba ni mali yako
 
Kibonho bongo hii haipo
Neno "bongo" linatumika kwa sasa kama sehem ambayo mambo yanafanyika old school na most hayaendi , na yakienda ujue unafanya illegal business au kua thief politician.
 
Back
Top Bottom