Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Nimewahi kuwa na account NMB sikuwa na matatizo nao sana, niseme ukweli tu. Ni miaka imepita tulikuwa na urafiki mzuri.
Nikawa NBC hawa walinikwaza kwenye kubadilisha card ya ATM ilichukua muda nikaachana nao.
Nikaja DTB nimefanya nao kazi miaka 3 ATM yao ika-expire. Nilifuatilia utadhani naenda omba kazi miezi mitatu. Nikaachana nao. Mbaya zaidi hata mikopo hawatoi kwa wateja. Wanatoa kwa Corporate tu. Nikaona upuuzi huo na kufuatilia ATM card utadhani nafuatilia kitambulisho cha NIDA. Nikaachana nao.
CRDB hawa hapa juzi juzi wamekuwa na wizi, wanatuibia wateja pesa kwa makato ambayo hayaeleweki. Watu wengi wamelalamika sana katika hili.
Sasa nauliza kwa wadau, benki gani inayomjali mteja. Kwao mteja anakuwa siyo tu Mfalme ila mteja ni Mume kabisa. Inatoa mikopo kirahisi, huduma nzuri, makato laini, inapatikana ndani na nje ya nchi maybe n.k
Ina kiwango rafiki cha kufungulia account, naweza fungua account na kupata ATM Card mapema tu bila usumbufu n.k.
Naombeni tusaidiane katika hili.