Mkuu, masharti ya benki nyingi ni karibia yanafanana, hii ni kutokana na ukweli kwamba benki kuu ndio wanasimamia uendeshaji wa hizi benki zote.
Kuhusu urahisi wa kufungua account kuna vigezo vingi kutikana na aina ya akaunti unayoitaka, kwa mfao:-
Akaunti yako ni ya kampuni au ya mtu binafsi, ni ya fedha za kigeni au za kitanzania, unataka upitishie mshahara au ni kwa ajili tu ya kuhifadhi hela zako? Kila aina ya hizo akaunti ina masharti yake.
Urahisi wa kufungua akaunti utategemea sana aina ya akaunti na wewe unataka kutumia huduma za kibenki kwa lengo gani?