Benki inaruhusiwa kupeleleza eneo lako la kazi unapoomba mkopo?

Joined
Sep 27, 2019
Posts
17
Reaction score
7
Habari wanajukwaa samahani naomba mbisaidie kuna ndugu yangu alienda kuomba mkopo Bank akapeleka nyaraka zake za kazini, yaani mkataba wa ajira pamoja na salary slips.

Sasa Bank ikaanza kumpeleleza katika eneo la kazi kitendo kilichopelekea kugundulika kwa wafanyakazi wenzake kuwa anataka kuchukua mkopo.

Je hii ni sawa mimi naona kama sio sawa maana ni kama Bank imevujisha taarifa za mteja wake au nyie mnaonaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bank kufuatilia ajira yako ni SAWA ili waingie mkataba na mwajiri wako nawe anakata moja kwa moja kwenye mshahara wako. Kwani hata kazini (Boss au wafanyakazi wenzako) wakijua kuna tatizo gani?
Bank ipo sahihi, maana wengi weshajaza mikopo kwa taarifa feki za kazi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana teyali mshahara unapita kwenye Bank yao it means wao watakata huko huko haina haja tena ya kusambaza hizi taarifa za mteja
Kuna ofisi nyingine zinatoa mokopo kwa wafanyakazi wake na wanapenda waone wafanyakazi wanachukua mikopo ofisini hapo sas huoni kama kuna kizuizi anaweza akapata huyu mtu katika kuchukua mkopo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Benki ni lazima iwasiliane na mwajiri wako, kumweleza kuhusu adhimio la mfanyakazi kuomba mkopo.

Ili mwajiri ahakikishe kwamba ataendelea kulipa mshahara kupitia hiyo benki.

Na wakati mwingine ni wao kutaka kujiridhisha kwamba una mkataba endelevu hapo kazini kwako.

Imagine, ukichukua mkopo kimya kimya halafu kumbe umeshatoa barua ya ku-resign, au ukamwambia mwajiri akubadilishie benki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…