Bwana Lole Gwakisa, ni kweli hujui benki zinatoa wapi Fweza???!!!
Jibu ni rahisi.. watu wanahifadhi hela zao huko benki.
Kwani benki inajiendeshaje kwa mfano kupata faida ya kuwalipa wafanyakazi,kulipia bili za umeme na simu???
Watu wanahifadhi pesa, wanalipwa riba kama 5% kwa mwaka halafu benki inakopesha kwa riba ya labda 10%. Hapo benki imepata faida ya riba 5%.
Swala ni kukopesa sio kugawa pesa. Kwa mfano mfanyakazi akikopeshwa, kila mwezi lazima apeleke kama elfu 50 kulingana na makubaliano.
Benking ni mzunguko wa pesa "money circulation"
hivyo kama benki ikikopesha watu wengi kwa riba ndogo inaweza kupata faida kubwa kuliko kukopesha watu wachache kwa riba kubwa, umeelewa hapo.
Shirikisho la Mashirika na vyama vinavyotetea masuala ya Makazi Tanzania (HAFOTA) wamesema wanaandaa mpango wa kuzibana benki kubwa kupunguza riba na kuongeza muda wa marejesho mpaka miaka 15.
Kwa mfano kama ukikopa Million 60, utalipa kama elfu 40 kwa mwezi. Hivyo basi, kila mtanzania ataweza kujenga nyumba bora.
Nawashauri hao Hafota waanzishe Petition, wapate Signature za watu wengi na hiyo itakuwa msukumo mkubwa sana. Kila atakaesaini aseme analipwa mshahara shs ngapi kwa mwezi na ataweza kurejesha kiasi gani kwa mwezi.
Wadau, toeni maoni Na kama mna mawasiliano na hao Hafota tafadhali wasilisha.
Mkuu Mpadmire,
Nadhani unaongelea masuala ya banking kwa kutilia maanani money circulation na si long term investment kama mbavyo mwanzoni uliligusia.
Mimi si mtaalam wa benki lakini kwa uzoefu mdago nilio nao najua kwamba
-Watanzania wengi si wawekaji wa amana katika benki kwa muda mrefu.
-wanopitisha hela zao za mishahara benki huzitoa ZOTE bila kubakisha
-benki zetu zinatoa riba NDOGO sanakulinganisha na inflation, hivyo kutovutia uwekaji wa amana.
Hivyo basi kutokana na benki nyingi kukosa UBAVU wa kukopesha LEO na ulipe taratibu kwa miaka 15, benki nyingi haziko tayari kukopesha kwa mtindo wa long term loans.
Hapa bado hatujaongelea RISK ya kibiashara, ya kukopa leo na kulipa katika muda wa miaka kama 15.
Kimsingi benki zetu zina fanya biashara ya kimachinga, biashara ya kupata faida leo leo.
Ili kujiondoa katika tatizo hili ni lazima benki zetu kwa kudhaminiwa na Serikali , zipate mkopo mkubwa toka mabenki makubwa ya uwekezaji.
Mbenki hayo yapo, ni serious ness ya wakuu wetu tu.
hizi banki zetu bado ni wavivu mbona benki zenye mitaji midogo kama azania na cba zinatoa mikopo ya nyumba.
azania
ukikopa 20m unalipa 323,000 kila mwezi for 10 yrs = 38.76m faida kwa benki 18.76m
ukikopa 30m unalipa 484,000 kila mwezi for 10 yrs = 58.08m faida kwa benki 28.08m
ukikopa 40m unalipa 645,000 kila mwezi for 10 yrs = 77.4m faida kwa benki 37.4m
ukikopa 50m unalipa 807,000 kila mwezi for 10 yrs = 96.84m faida kwa benki 46.84m
kwa hiyo gwakisa utaona faida bado ni kubwa sana mabenki yatapata hata ukiangalia ulaya mabenki mengi yanaendeshwa na mortagage
kadri unavyokaaa na hela yao kwa mmuda mrefu... riba ndo inaongezeka...!!Mbona faida kubwa sana? yani ni kama BAYPORT na zile SACCOS za mtaani!