Tetesi: Benki Kuu kuzuia wafanyakazi wake kusoma Open University of Tanzania

Tetesi: Benki Kuu kuzuia wafanyakazi wake kusoma Open University of Tanzania

Bara na pwani

New Member
Joined
Jan 2, 2014
Posts
2
Reaction score
9
BENKI KUU KUZUIA WAFANYAKAZI WAKE KUJIUNGA NA OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA

Katika mazungumzo na mfanyakazi mmoja wa benki kuu ya Tanzania ambae ni mhitimu wa masomo ya shahada ya uzamivu katika chuo cha Open University of Tanzania (OUT), nilimwomba ushauri wake kuhusu elimu wanayotoa pale OUT huku name nikiwa na nia ya kujiunga na chuo hicho.

Hata hivyo katika hatua ya kushangaza aliniambia kwamba yeye ni katika wanafunzi wa mwisho mwisho kusoma pale OUT, maana alipoingia Gavana mpya Prof. Luoga alianza kwa kuzuia wafanyakazi kwenda kuongeza elimu mpaka ajiridhishe mahitaji na vyuo watakavyosoma.

Mwaka 2018 haikutoka ruhusa ya kwenda shule, mwaka 2019 akatoa mwongozo wa vipaumbele na vyuo vya kusoma ambapo OUT ilizuiwa na wanafunzi waliotaka kwenda kuongeza elimu walishauriwa hasa kwenda UDSM.

Open University of Tanzania ni chuo cha serikali na kiliundwa kwa mara ya kwanza kwa nia ya kusaidia watu ambao wanasoma kwa njia ya mtandao lakini baada ya muda kimekuwa chuo tegemezi kinachotoa kozi kwa wanafunzi kuhudhuria darasani. Ikumbukwa hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesoma hapo, iweje chuo hiki kidharaulike.

Kuna haja ya uongozi wa benki kuu kujirekebisha na kuacha kubagua elimu za vyuo vyetu, kama kuna mapungufu kuna njia za kutoa maoni ili TCU wafanye uboreshaji wa mitaala yao. Kwa hili nawashauri benki kuu wajirekebishe
 
Yaani ww ni kilaza kabisa unachukuwa ma azo ya mtu mmoja then unaya "generalized" stupid
 
Hata udsm watu wanafanyiwa tunajua madokta hawakuandika hata one page na wapo walimeza tuu wakati boa. Sio leo wala jana.
Mmoja MAGUFULI.

Dah Ben Saanane ilimgharimu baada ya kuweka huu ukweli.
 
Open University of Tanzania ni chuo cha serikali na kiliundwa kwa mara ya kwanza kwa nia ya kusaidia watu ambao wanasoma kwa njia ya mtandao lakini baada ya muda kimekuwa chuo tegemezi kinachotoa kozi kwa wanafunzi kuhudhuria darasani. Ikumbukwa hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesoma hapo, iweje chuo hiki kidharaulike.

Kuna haja ya uongozi wa benki kuu kujirekebisha na kuacha kubagua elimu za vyuo vyetu, kama kuna mapungufu kuna njia za kutoa maoni ili TCU wafanye uboreshaji wa mitaala yao. Kwa hili nawashauri benki kuu wajirekebishe
Kimeumana
 
Back
Top Bottom