Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuwa malipo ya benki moja kwenda nyingine yanapaswa kukamilika ndani ya saa mbili, na ikiwa mteja hajapata fedha yake ana haki ya kuishtaki benki husika kwa kuwa analindwa na sheria.
Akiwasilisha mada ya mifumo ya fedha, Ofisa Mwandamizi Mkuu, Mifumo ya Malipo ya Taifa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kidee Mshihiri, amesema mfumo wa kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine unaitwa Interbank Settlement System (TISS) ambao umeimarishwa.
Soma, Pia: Hizi ndizo noti zitakazoondolewa kwenye mzunguko kuanzia Januari 06 hadi Aprili 05 mwaka huu
Amesema kumekuwa na tabia ya mteja kuambiwa tatizo liko BoT ndio maana hapati malipo yake, jambo ambalo si kweli kwa kuwa BoT inaona tu haiwezi kufanya chochote kwenye muamala wa mtu kwa kuwa benki zote za biashara akaunti zao zipo Benki Kuu.
"Unakuta mtu ameenda benki X amehamisha fedha kwenda benki nyingine akifika kule anaambiwa hakuna fedha, akirudi kwenye benki alitohudumiwa anaambiwa tatizo liko BoT, jambo ambalo si sahihi. Ukiamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine lazima ndani ya saa mbili upate," amesema.
CHANZO: Nipashe