Tausi Afrika Yazindua Mfumo wa Kiotomatiki wa Uchambuzi wa Kifedha kwa Kutumia Akili Bandia
Kampuni ya Tausi Afrika imeleta mfumo mpya wa uchambuzi wa kifedha uitwao MANKA, ambao unatumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kusaidia taasisi za mikopo.
Mfumo huu unawawezesha watoa mikopo kuchambua taarifa za kifedha kutoka benki na simu kwa haraka, na hivyo kupunguza muda wa tathmini za mikopo.
MANKA umelenga kutoa suluhisho la haraka na sahihi kwa taasisi za kifedha, kurahisisha maamuzi ya kifedha kwa kutumia data kamili na ya kuaminika kwa muda mfupi.