Benki ya CRDB yapunguza viwango vya riba ya mikopo na kuongeza muda wa marejesho kwa watumishi

Benki ya CRDB yapunguza viwango vya riba ya mikopo na kuongeza muda wa marejesho kwa watumishi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
pic+crdb.jpg

Dar es Salaam. Benki ya CRDB imeongeza muda wa marejesho kutoka miezi 60 hadi 84 huku ikishusha riba kwa asilimia nne kwa wateja wake, hasa wafanyakazi.

Benki hiyo imeshusha riba kutoka asilimia 21 mpaka 17 huku muda wa marejesho ukitofautiana kati ya wafanyakazi wa sekta binafsi na watumishi wa umma.

Wateja wa benki hiyo wameanza kunufaika na punguzo hilo tangu wiki iliyopita pindi menejimenti iliporidhia kufanya mabadiliko hayo.

Akizungumza na Mcl Digital leo Mei 13, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk Charles Kimei amesema mabadiliko hayo yanalenga kumpa mteja unafuu wa kukamilisha malengo yake kwa wakati.

“Punguzo hili linatolewa kwenye matawi yetu yote. Tangu wiki iliyopita huduma hiyo imeanza kupatikana,” amesema Dk Kimei.

Watumishi wa umma ambao awali walikuwa wanafanya marejesho mpaka miaka sita ambayo ni sawa na miezi 72, sasa wanaruhusiwa kufanya hivyo mpaka miezi 84 au miaka saba wakati wafanyakazi wa sekta binafsi waliokuwa na miaka mitano wameongezewa mpaka miaka sita.

Hatua ya CRDB imekuja baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kushusha riba ya mikopo inayotoa kwa benki za biashara mara mbili mfululizo.

Machi mwaka jana, ilipunguza riba hiyo kwa asilimia nne kutoka asilimia 16 mpaka 12.

Mwaka mmoja baadaye, BOT ilipunguza tena kwa asilimia moja na kushusha kiwango cha akiba ambacho benki hizo zinatunza kwake kutoka asilimia 10 mpaka nane ili kuzipa uwezo zaidi wa kuikopesha sekta binafsi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa hili Magufuli anastahili pongezi. Hizi benk za biashara zilikua zinafanya kazi na serikali na sio wananchi wa kawaida.

Serikali ilikua inazilipa riba kubwa sana kwenye mikopo yake, 15-16%, kwa hiyo wakawa wanaona bora kufanya biashara na serikali kuliko watu binafsi.

Sasa serikali imepunguza riba ya mikopo yake, toka 16% hadi 6%.

Sasa benk zote itabidi zipunguze tu hakuna namna. Nangoja NMB, sasa wako 18%, warudi 16% au 15% watu wakope.

Hizi riba zinapaswa kua chini ya 15%.

Hongera Dr. Magufuli.
 
Uzembe tu... mtu msomi umesoma kabsa unaenda kopa eti unaacha atm card mwsho kudhalilishwa mtaani
.
Kumbe unaipata hiyo mkuu!
Wakati mwingine hata wastaafu wanaingia mkenge yaani Kuna kipindi niliwaonea huruma sana!
Mtu anasubiri mafao yake ila jamaa kashatega 20 million ni zake!

Hatari sana
 
Duh, hiyo kweli kali, mkopo wa miaka saba hiyo riba yake ni balaaaaaaaa, ila kwa utawala huu, bora uchukue pensheni yako mapema uwekeze, mambo mengine yatajiseti baadae
 
Kwa hili Magufuli anastahili pongezi. Hizi benk za biashara zilikua zinafanya kazi na serikali na sio wananchi wa kawaida.

Serikali ilikua inazilipa riba kubwa sana kwenye mikopo yake, 15-16%, kwa hiyo wakawa wanaona bora kufanya biashara na serikali kuliko watu binafsi.

Sasa serikali imepunguza riba ya mikopo yake, toka 16% hadi 6%.

Sasa benk zote itabidi zipunguze tu hakuna namna. Nangoja NMB, sasa wako 18%, warudi 16% au 15% watu wakope.

Hizi riba zinapaswa kua chini ya 15%.

Hongera Dr. Magufuli.
Aongeze mishahara ili watumishi wakopesheke zaidi. Hizo riba bado ziko juu mtu kukopa na kufanya jambo la maana kwa mishahara ya baadhi ya watumishi serikalini hasa wa ngazi za chini na ambao ndio wengi.
 
Mikopo ni janga ni maumivu ya Taifa
Hicho ni kitanzi wakuu, ngoja wafanyakazi wauingie mkenge wenyewe hasa bila nyongeza ya yoyote ktk take home, wakumbuke kuwa mchuma janga hula na wa kwao
 
Hongera JPM watakuelewa tu.
Bank zilikuwa zinatumia fedha ya Serikali kuikopesha Serikali
 
Back
Top Bottom