Benki ya Dunia kuipa Tanzania Tsh. Bilion 348.9 kusaidia mabadiliko ya kidigitali

Benki ya Dunia kuipa Tanzania Tsh. Bilion 348.9 kusaidia mabadiliko ya kidigitali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Benki ya Dunia inatarajia kutoa dola milioni 150 sawa na takribani Tsh. Bilioni 384.9.

Fedha hizo zinatolewa kwa ajili ya kusaidia mabadiliko ya kidigitali nchini. Waziri amesema fedha hizo zitaboresha upatikanaji wa huduma za intaneti ili kukuza uwezo wa serikali kutoa huduma kwa kidijitali.
 
Hili linchi, wanajali maendeleo ya vitu kuliko ya watu! Hayo mamikopo yote watarudishaje?
 
Lazima Serengeti bandari lake Victoria na ardhi iridushwe kwa makaburu ama mabepari. Mtalipaje hii mikopo yote.
Ila nchi hii sidhani Kama miaka Mia itapita kunuka Kama watalebani Hezbollah,
 
Hizi hela huwa zinaenda wapi mbona mawasiliano bado mabovu?

Huwezi amini kuna mahali ukienda nchii hii huwezi hata kutuma meseji.

Lakini mapesa yanamwagwa tu!!
 
Kikwazo cha mabadiliko na maendeleo ya kidigitali yamekuwa yanazuiwa na Serikali..., yaani hata bila hizo pesa Serikali isingeweka vikwazo tungekuwa mbali zaidi.... Case Studies..

Kipindi Skype imekuja na watu kuweza kuongea kwa kutumia internet na watu wa nje, Serikali iliweka vikwazo Tanzania (eti TTCL atakosa mapato)

Watu wote mpaka vijijini walishazoea kutumia digital wallet (mpesa, tigo et al) yaani mtu hata alikuwa akiwa chumbani anataka kumtumia mtu pesa yupo sebuleni anatumia digital money sasqa hizi tozo zimeturudisha kwenye kutuma pesa kwa bahasha...

In short kusaidia maendeleo ya kidigitali Serikali ingeacha tabia yake ya kufix things while they aint broken ingesaidia zaidi, sio hii mikingamo ya Pwagu na Pwaguzi....
 
Back
Top Bottom