Benki ya Dunia yaisadia Tanzania dola milioni 300 kuendelea kuimarisha sekta ya nishati nchini

Benki ya Dunia yaisadia Tanzania dola milioni 300 kuendelea kuimarisha sekta ya nishati nchini

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
TANZANIA KINARA AFRIKA KWA USAMBAZAJI WA NISHATI KWA WANANCHI

IMG-20240604-WA0009.jpg

📌 Tanzania na Benki ya Dunia kushirikiana katika miradi ya nishati

📌Benki ya Dunia yaisadia Tanzania dola milioni 300 kuendelea kuimarisha sekta ya nishati nchini

📌Tanzania yapongezwa kufanya vizuri usambazi wa umeme kwa wananchi

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

IMG-20240604-WA0010.jpg

Tanzania imepongezwa na Benki ya Dunia kwa kuwa miongoni mwa nchi inayoongoza kusambaza Nishati ya Umeme kwa wananchi wake

Akizungumza leo Juni 4, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameishukuru Benki ya Dunia kwa pongezi hizo na kusema kuwa Benki hiyo ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na kuwa wamekuwa na ajenda ya kushirikiana katika miradi ya nishati.

IMG-20240604-WA0011.jpg

“Tumefurahi kusikia nchi yetu imepiga hatua na tumejipanga kuendeleza miradi mingine ya nishati ili kuhakikisha kuna utoshelevu wa Nishati hiyo nchini", amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza “Tutaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza kila fedha tunayopata lazima iwe na thamani kwa wananchi. Wizara pamoja na Shirika letu la umeme TANESCO limepongezwa kwa kushughulikia vizuri suala la nishati nchini, hata hivyo ni lazima kuangalia mbali zaidi si tu kuridhika kwa hapa tulipofika.”

IMG-20240604-WA0013.jpg

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete amesema kuwa Benki hiyo inatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfumo mzuri wa kusambaza nishati kwa Watanzania.

“Hapa Afrika, Tanzania ni mfano mzuri katika usambazaji wa Nishati ya Umeme kwa wananchi. Tumejipanga kuwa na mazungumzo zaidi na kuona namna bora zaidi ya kusaidia katika masuala ya nishati safi ya kupikia kwa kufadhili na kuhusisha sekta binafsi kwa kuangalia fursa zilizopo”, amesema Belete.

Aidha, Bw. Belete amesema kuwa Benki hiyo inatoa fedha kiasi cha dola za kimarekani milioni 455 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 ukutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Ameendelea kwa kusema kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuiendeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.
 
Duh! Pamoja na DP world bado tunakopa na kusaidiwa.
Ukifuatilia katika lugha za hawa watu, na hasa hawa WB, wanasisitizia sana "sekta Binafsi"; lakini husikii chochote wakisema hiyo sekta binafsi ni ya wapi, na wala hawajishughulishi vyovyote na kukuza hiyo sekta hapa hapa nyumbani!
Kwa hiyo maana yake ni kuwa tukatafute 'sekta binafsi' toka nje, waje hapa kutufanyia mambo yote ya umeme na sehemu zinginezo.

Bila shaka mfano wao mzuri wa mkopo waliotupatia ni wa kukarabati Bandari, ambayo baada ya kuiboresha, tukawaita sekta binafsi, DPWorld kuja kuchuma.
Huu ni uhayawani.
 
Kwanza kabisa tumshukuru mola tunakopesheka, na tunasaidika...
Pili nguvu kubwa tuwekeze kwenye maombi ili walio tukopesha wasahau kutudai...
Au mnasemaje watz wenzangu。
 
Kikubwa mikopo hii itumike vizuri! Ubaya ni pale Mh anapokuwa legelege kusimamia fedha ili zisiishie mifukoni mwa wajanja!
 
Back
Top Bottom