Benki ya Dunia yatoa mikopo ya nyumba ya Sh50 bilioni

Hakuna kitu hapo, hizo pesa zitaishia kwenye mifuko ya watu wachache tu, na mzigo wake tutaubeaba walala hoi.naona pesa hizo ni maalumu kwa kampeni ya CCM, hakuna nyumba wala nini!.ni usanii ule ule tuliouzoea.
 
sasa naona haya ndio aliozungumzia Game Theory kwenye issue ya ufisadi wa kumchagua yule ceo nhc.mambo yamekamilika bilioni 51 hio watu udenda unawatoka.
 

Kaka ukizungumza fikiria kama uko tanzania usifikirie uko nje ya tanzania. Jiulize ni mikopo mingapi Tanzania imechukua imeleta natija kwa Tanzania. Tunasikia tumekopesha bilioni 20 kwa ajili maendeleo ya technolojia, mara tumekopeshwa bilioni 10 kuendeleza miradi ya maendeleo, mara tunakopeshwa kwa ajili ya pembejeo.

Swali je hizo pesa zimefanikisha maendeleo mangapi au maendeleo ni kubadilisha magari ya miradi (mfano tuna malandcruiser ya 2010 katika miradi sijui yanafanya nini? yale ya zamani yameenda wapi?). usimamizi wa miradi upo? na kama upo je miradi iliyofanikiwa mingapi? au ndio pesa zinaishia nusu katika mifuko ya watu??? Halafu taifa linaishia kulipa deni maendelo hakuna
 
sasa naona haya ndio aliozungumzia Game Theory kwenye issue ya ufisadi wa kumchagua yule ceo nhc.mambo yamekamilika bilioni 51 hio watu udenda unawatoka.

Mzee ndio nikaomba Game theory atuhabarishe inakuwaje?
 
Mmeshachelewa.. tayari hii habari ilishaanza kufanyiwa kazi tangu end o the year last year baada ya taarifa kutoka. Tayari makampuni mapya ya Real Estate yameshasajiliwa na contact za Benki Kuu zimeshawekwa na miongoni mwa wenye makampuni hayo makubwa ni wale walioko kwenye serikali ya sasa.. kama mnafikiri Mkapa na mwenza wake wana control real estate mtakoma mwaka huu!!
 

Uwii!!!
 
hii tabia haitaisha kwa vile hakuna mtu anayechukuliwa hatua yoyote.kwanini watu hawachukuliwi hatua? kwa vile hakuna msafi wa kumchukulia hatua mwenzake.
 
Naona wanajifikiria badala ya kuchota 30% au 20% ya hizo hela labda wachote 10%- 15%

Naona wanahaha kufikiria ni njia gani watacheza faulo bila sisi watazamaji kuona wanaanza kuona. Maana miwani ya jua waliyutupa kutazamia tuemeweka pembeni.

Naona JF imemuanika REFA( CEO) na sasa kazi ya kuwapa WALE ushindi sio rahisi sana.

Watazamaji tusilale hata kuzomea pale refa atapochemsha kunasaidia. na Refa akichezesha kwa haki tumpe hongera zake.
 
Rai yangu hizi pesa zitumike kama ilivyopangwa.Zisiwe allocated to other activities na kutoa excuses kibao.Fedha ziwafikie beneficiries.
 

Watakapogundua hili liinchi linavyoliwa ndio watakapojua kwamba madudu ya che-Nkapa ni cha mtoto. Ka-nchi bado kanaendelea kunuka rushwa na uvundo wake unanuka hadi NY.
 

Kwakweli inakatisha tamaa..........tutafika tu
 
Tanzania na ulimwengu wa siloviks, ambao Bolis Yetsin aliutengeneza baada ya kuanguka kwa USSR. Ni family yake tu na wapambe ndio walionekana kujua biashara. Wabunge na wapinzani walikuwa wanahongwa ili kumpamba rais huyu .
Yaani watu wale wale tu kila kona.Ipo siku haya yatafika mwisho.
 
wait for the exclusive story inayokuja next week... hawa watu watakula hili taifa kama mchwa kwenye nyumba.. Kama nyumba affordable ni kama za Gavana na Manaibu wake.. sijui mtasemaje..

Serikali hii hii imeacha kina Yona wajitoe kwenye mradi wa Wamarekani ambao walitaka kuja kujenga nyumba 5000 within 2 years kwa sababu wamesikia dili hii mpya..

don't get me started...
 
Hawa WB wanachekesha kweli! Yaani hadi leo hawajajua kuwa hii mikopo haifiki kokote? Hawana nia ya kutusaidia kabisa hao, ni biashara tu.
 
Hawa WB wanachekesha kweli! Yaani hadi leo hawajajua kuwa hii mikopo haifiki kokote? Hawana nia ya kutusaidia kabisa hao, ni biashara tu.

We jiulize kwanini mabenki yote ulaya yanakuwa in one way or another involved na african countries particularly in conflict areas. The biggest business for these guys ni interest nchi maskini zinalipa katika mikopo yao na rasilimali zetu. Sasa kwakuwa wanajua fika kwamba zile si lolote wala si chochote wanamezea mate na kuuchuna huku wao wanavuta faida.

Wakiona wazawa tumeng'aka sana wanajidai kutingisha kiberiti baadae wanawaachia. Wanafahamu Tanzania ina report mbovu ya utawala bora wametoaje mikopo kama hii??
 
Kwa wale wanaojua magari mazee ni kwamba inafika mahali kila unapogusa ni pabaya. Inabidi kulibadilisha, sio kulikarabati.

Hapa tulipo serikali ya CCM haikarabatiki, kwani kila mahali pameoza. Ni ya kubadilisha. Inatumia wananchi masikini kuomba mikopo ya kuwanufaisha wakubwa tu!

Tunao uchaguzi mwaka huu. Tukichagua tena CCM basi tuwe na uhakika wa kuendelea na hali ya sasa, au hata hali mbaya zaidi. Tukitaka kubadilika, lazima kubadilisha serikali. Imewezekana huko Zambia na kwingineko, kwanini ishindikane kwetu?

Hakuna Mtanzania yoyote masikini ambaye hali yake itabadilika awe na nyumba kama tutaendelea na serikali ya sasa. Hata tukikopa wapi ni bure tu.
 

Kwa kweli inatia masikitiko na mshangao kwani haijapita hata muda tangia kijana achaguliwe (MCHECHU) THEN yaliyotabiriwa yanatimia ya hela za uchaguzi. tulidhani kijana anaenda NHC kuondoa ufisadi na wizi uliojaa kumbe anaenda kuendeleza jahazi. wako wapi wanolinda maslahi ya umma?
 
dili kama kawaida mwenye nacho ndo uongezewa hiyo ndo fomula habari ndo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…