SoC04 Benki ya Vijana na wajasiriamali suluhisho la mitaji na uwekezaji kwa miradi ya vijana

Tanzania Tuitakayo competition threads

WAPEKEE_

Member
Joined
May 23, 2024
Posts
21
Reaction score
28
Hatimaye kila kijana anapenda biashara, kila kijana anafanya ubunifu wa wazo la biashara na bidhaa, sasa ujasiriamali sio dhana ya wale akina mama wanaotengeneza zile sabuni nyeusi nyeusi za vipande bali ujasiriamali wa sasa unachukuliwa kama dhana ya vijana waliothubutu kujiajiri na kupewa cheo cha heshima cha Mjasiriamali. Sasa vijana tumeuelewa Ujasiriamali na tumeupenda na tunaufanya.

Ujio wa mitandao ya kijamii, umerahisisha vijana kufanya biashara kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hata kama vijana hatuna bidhaa, maduka, na mitaji lakini sasa tumeamua kuwa ‘Mawinga’ ( Watu wa Kati ) kwa kuwaunganisha wafanyabiashara na wateja , ambapo imetusaidia kuwa na ule ujasiri na uthubutu wa kuamini kwenye kufanya kazi na ujasiriamali kwa ubunifu wa bidhaa zetu.

HALI YA MITAJI NA MIKOPO
Ni ukweli usiopingika kuwa bado asilimia kubwa ya watanzania ni maskini, na vijana wengi tunatoka familia maskini ambazo hazina uwezo wa kuwawezesha vijana wake kwa kuwapa mitaji ya kifedha za moja kwa moja Katika kuwawezesha mawazo yao ya biashara, na kufanya vijana wengi wasiweze kuanzisha biashara na kuzisimamia kupita kwenye mitikisiko ya kupanda na kushuka.

Upatikanaji wa mitaji umekuwa mgumu kwasababu taasisi nyingi za kifedha na mikopo, zinahitaji dhamana ambazo kimsingi vijana wengi hawana dhamana na kukosa sifa za kukopesheka.
Serikali imekuwa na utaratibu wa kuwakopesha vijana kupitia halmashauri za wilaya, miji na majiji, ambapo asilimia kumi ya makusanyo ya ndani yanapelekwa kwenye kuwakopesha vijana, wanawake na walemavu. Napo hawakopeshwi kijana mmojammoja bali wakiwa kikundi tu, na kwenye vikundi nako kuna changamoto nyingi sana ikwemo kutofautiana mawazo na ufanyaji wa biashara na miradi.

Hatahivyo mpaka naandika andiko hili tarehe 26 Juni 2024, pesa hizo zilikuwa zimesitishwa kwa takribani mwaka na kuahidiwa kuwa zimerudi lakini ulikuwa unasubiriwa utaratibu mpya wa kupata mikopo hiyo na mpaka naandika andiko hilo bado pesa hizo hazikuwa zimeachiliwa na hata baada ya kuachiliwa zingetoka kwa halmashauri chache tu za majaribio.

Pia halmashauri zisizokuwa na ukusanyaji wa mapato makubwa na hasa zile za vijijini hazikidhi mahitaji kwa idadi ya vijana wanaotaka kujiajiri kwa ujasiriamali.

Amini msiamini, hivi sasa kuna utitiri wa mikopo mtaani, maarufu kama kausha damu, kuna utitiri wa Aplikesheni za kimtandao ambazo zinakopesha kweli japo kwa riba kubwa, lakini wanakopesha kweli na wakianza kudai, mpaka utatoa mwenyewe kwa njia zao, japo sio njia sahihi kisheria lakini utalipa tu deni namimi ni shahidi wa hilo.

Ndugu zangu kama Mikopo kausha damu na Aplikesheni chefuchefu zimeweza kukopesha, kudai na kupata faida yao , hivi kweli serikali yetu tukufu itashindwa kweli kuanzisha Benki ya muda wote ya kutoa mikopo kwa vijana na wajasiriamali na kurejesha pesa zake hata kwa faida ikitakaa?

BENKI YA VIJANA TANZANIA, SULUHISHO LA KUDUMU.
Kwa maslahi mapana ya maendeleo ya kisekta kama vile, kilimo na wanawake , serikali na wadau wa maendeleo , Walianzisha na kupewa mitaji na usimamizi wa Benki maalumu za kisekta. Mfano mpaka sasa Benki ya kilimo imeongezewa mtaji na serikali kutoka bilioni 60 mpaka bilioni 435.4 kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi mwaka 2023/2024 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 625. Hio imesaidia upatikanaji wa rasilimali fedha, ongezeko la mtaji na mazingira rafiki ya utendaji yaliyowezesha Benki kufikisha huduma kwa wakulima wengi nchi nzima na kuinua maendeleo ya kilimo Tanzania.

Kama sekta ya kilimo ina benki yeke, Vijana ambao ndio nguvu kazi kwenye kilimo na sekta zote za maendeleo , kwa ulazima na makusudi, ianzishwe Benki ya vijana malumu kwa Mitaji, Mikopo, Usajili, Biashara, Kutambulisha na kuwaunganisha vijana wote wa Tanzania, kuanzia kwa wana taaluma, wafanyabiashara, wakulima, wachimbaji wa madini, wabunifu, wanasanaa, wanasayansi, wajasiriamali na wote wenye shauku ya maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Benki hii itawafikia vijana wote wa Tanzania na hata walio nje ya Tanzania. Benki hii itakuwa mahususi kwa vijana na haitakuwa na mipaka au vikwazo vya kuwahudumia vijana nchi nzima. Hata katika bajeti za nchi itakuwa inapewa bajeti zake kisheria na kuendeshwa kitaasisi zaidi ili kulinda maslahi yeke kwa kuiendesha kifaida zaidi kwa kuwawezesha vijana na kurudisha faida kwa kupitia Mikopo, Magawio, Miradi, Marejesho, Riba (Riba Za Asilimia ndogo) na mikakati ya kimaendeleo kupitia benki hiyo maalumu kwa vijana na wajasiriamali.

SHERIA YA UENDESHAJI WA BENKI HIYO.
Zipo wizara maalumu kwa vijana kama vile Wizara ya Kazi, Ajira na maendeleo ya Vijana. Pia ipo Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambayo ina wajibu wa moja kwa moja kwa vijana. Ipo wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu ambayo vijana pia wamo. Kule zanzbari ipo Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo. Pia upo mkakati wa kuanzishwa kwa Baraza la Vijana Tanzania huku ikiwepo Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania pamoja na Sera ya Taifa ya Vijana.

Ukiangalia vyombo vyote hivi , vina nguvu kubwa ya kuianzisha kisheria Benki ya Vijana kwa maendeleo ya vijana Tanzania. Benki hii iwe kitaasisi tena Taasisi ya Umma itakayolindwa kisheria vizazi kwa vizazi.

Benki hiyo itasaidiana na benki zingine za kisekta kama benki ya kilimo na benki za taifa za biashara kama vile TCB nakadharika. Suala la kuwawezesha vijana halipaswi kuwa suala la hiyari, bali suala la lazıma.

ELIMU YA FEDHA NA BIASHARA
Benki hii , itakuwa na majukumu ya kutoa Elimu ya Fedha, Biashara, Uwekezaji na Ubunifu kwa kuwawezesha vijana kuwa na sifa za kuingia kwenye soko la ushindani wa biashara na ubunifu . Elimu ya Fedha kimatumizi, uwekezaji na Akiba ni moja ya changamoto kwenye mtindo maisha wa Vijana ambao umebeba uhai wa maisha ya jamii. Vijana wapewe elimu ya Ubunifu wa sanaa na bidhaa za kipekee zitakazoingia sokoni na kupata faida kubwa, hapa watashirikiana na Vyuo Vya Ufundi, Taasisi za Sayansi na Teknolojia, na Vikundi vya Uzalishaji mali.

MWISHO
Masuala ya vijana hayapaswi kuendeshwa kisiasa, bali kitaaluma na weredi. Benki hii iendeshwe na wasomi wenye taaluma juu ya Uchumi na Fedha. Na ndio mana Serikali imeamua kuliweka suala la asilimia kumi ya halmashauri , zitolewe kwa mfumo wa Benki ili taaluma na weredi vifanye kazi ili kuleta matokeo ya kweli. Napendekeza benki ya Vijana iundwe kulinda maslahi ya Vijana kwa vizazi vijavyo na kwa Tanzania Bora Tuitakayo kwa miaka 25 ijayo .

WAPEKEE KEPHAS YOHANA SIMU : +255 694 024 888 / +255 746 623 366 / +255 674 968 400 / +255 684 193 588
 
Upvote 2

Umeandika vyema sana . BENKI ya vijana itakuwa ni suluhisho
 
Back
Top Bottom