nabii7y7
New Member
- Jun 12, 2023
- 3
- 3
UTANGULIZI
Kwa dunia ya sasa ambayo imepiga hatua sana katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kuongeza ushindani katika uzalishaji wa bidhaa muhimu za binadamu na wanyama wengineo ili kukidhi uhitaji unaoongezeka kila siku na kila kona ya Dunia, hatuwezi kusahau umuhimu na mchango wa sekta ya fedha katika kuleta matokeo chanya katika sekta ya kilimo.
Bila kusahau kubwa kilimo ni sekta ambayo ni uti wa mgongo katika nchi nyingi za ukanda wa kusini mwa Afrika na Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizi ambazo zaidi ya asilimia sitini ya wananchi wake tunategemea kilimo kukidhi mahitaji yetu ya kila siku, hapa namaanisha chakula na kipato kwa pamoja.
Pamoja na kilimo kuwa uti wa mgongo kwa uchumi wa nchi yetu na kuleta matokeo chanya kiujumla na serikali, wadau binafsi pamoja na makampuni kujitolea kuwekeza katika sekta hii muhimu sana, lakini imekuwa ndio sekta iliyokosa uwiano katika upatika wa mitaji na kwa wakulima wadogo wadogo katika maeneo mengi ya vijijini.
Japokuwa zimeanzishwa Taasisi mbalimbali za kifedha zikiwemo benki ambazo asilimia kubwa mkono wa serikali unahusika moja kwa moja na lengo likiwa ni kuinua na kuiendeleza sekta ya kilimo nchini ili kukidhi ushindini wa kimataifa, lakini taasisi hizi zimekosa kuaksi uhalisia wa mkulima wa kijijini na huduma zinazotolewa mjini.
Mfano: Ukiangalia asilimia kubwa ya wakulima
Wanapatikana maeneo ya vijijini lakini huduma nyingi za benki za kilimo zinapatika mjini ambako ni vigumu sana kwa wakulima wadogo wadogo kuzifikia pindi wanapozihitaji.
Sambamba na hilo masharti na vigezo vinavyotumika kutoa huduma hizi kwa wakulima wadogo wadogo zimekosa ufanisi na uhalisia wa kuanzishwa kwake.
Pia mzunguko anaotakiwa kupitia mkulima ili kupata mkopo katika benki hizi unakosa uhalisia wa kimkakati swala linalorudisha maendeleo yaliyofikiwa kutokuwa endelevu na kufifisha mafanikio ya kimkakati miongoni mwa wakulima wa vijijini nchini.
Kwa mfano: Ni wakulima wangapi ambao wanaweza kujidhamini ili kupa mkopa kutoka taasisi za kifedha zinatoa mikopo kwa ajili ya kilimo na kukidhi vigezo zikiwemo benki za kilimo?
Au ni wakulima wangapi wanaweza kufunga safari kutoka vijijini kuja mjini ili kupata huduma hizi?
Lakini pia taasisi hizi zimeandaa mazingira gani rafiki ili kuhakikisha kuwa wakulima wadogo wadogo wanaweza kupata huduma hizi kwa urahisi ili kumuondolea sumbufu mhitaji?
Pamoja na juhudi nyingi zinazofanywa kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa kilimo kinanufaisha mkulima hata yule ambaye yupo mbali na maeneo ya mjini lakini bado changamoto ni nyingi ambazo zinaondoa ufanisi katika sekta hii.
USHAURI WANGU
Ni wakati sasa wa Taasisi hizi za kifedha zinazotoa huduma za kifedha kwa wakulima kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja na wakulima kutoka maeneo husika hasa vijijini ili ziweze kuwafikia walengwa kwa urahisi.
Benki za kilimo na taasisi zinazohusika zianzishe ofisi dogodgo maeneo ya vijijini na kupeleka wataalamu waliobobea katika uchumi wa kilimo ili kukidhi uhitaji wake kwa wakulima.
Serikali iingilie na kutathmini ufanisi wa baadhi ya taasisi za kifedha ambazo zimeanzishwa na watu binafsi na makampuni fulani fulani ambazo zimegeuka kuwa kikwazo na mwiba kwa wakulima ikiwemo kuwatapeli na kuwanyonya wakulima hasa vijijini.
Serikali kama mdau mkuu katika kuhakikisha kubwa mkulima anapata huduma bora basi ije na mpango kazi wa kuongeza ushindani miongoni mwa benki za kilimo katika kuwahudumia wakulima na kuwafikishia huduma walipo baada ya wakulima kuifuata huduma mjini.
Wizara ya fedha na wizara ya kilimo kwa pamoja zianzishe programu ya kupokea maoni ya huduma za kifedha zinatolewa na taasisi husika kutoka kwa wakulima wadogo wadogo badala ya kutumia wakulima wakubwa na makampuni ya kilimo kutoa tathmini zao.
HITIMISHO
Ili tuweze kufikia malengo ya kuwa na maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo nchini na kukidhi mahitaji ya msingi katika sekta hii ambayo ni uti wa mgongo kiuchumi, ni lazima nchi iwe na mipango inayotekelezeka ikijumuisha mipango ya muda mfupi na na ile ya muda mrefu.
Pamoja na hilo ni vema sasa wizara ya kilimo kuwaandaa wakulima kuendana mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo kutumia mbegu za kisasa zinazohimili mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuepusha hasara zisizo za lazima kwa wakulima wadogo wadogo.
Mwisho napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wadau mbalimbali wenye elimu ya kilimo biashara pamoja na serikali kuhakikisha kuwa pamoja na changamoto zote zinazowakabili wakulima wadogo wadogo, watoe elimu ya mikopo ya kilimo kwa wakulima wadogo wadogo ili kukuza uelewa miongoni mwa wakulima ili waweze kuingia kwenye soko la ushindani ili kuleta maendeleo endelevu nchini.
Asanteni sana.

Upvote
1