Benki za NMB,POSTA na CRDB kutonunua madeni ya wafanyakazi wanaotaka kukopa sio urasimu na kubweteka?

NENDA CRDB WANANUNUA MIKOPO YA TAASISI NYINGINE LAZIMA WAANDIKE BARUWA YA KUOMBA TAARIFA YA MKOPO KWENYE BENKI NYINGINE WAKIJIBIWA BASI UNAPEWA CHAKO KINGINE WANALIPA BENKI HUSIKA
Basi ndio watakuwa wameanza hivi karibuni kama ni kweli unachosema.
 
Nafikiri kila taasisi ya kifedha huwa na requirements zake, (Buy back) si kila taasisi inakuwa nayo. Na kwa vile kwa sasa tuko kwenye ushindani, binafsi naichukulia hiyo si urasimu kama ambavyo mtoa hoja unaichukulia. Hii ni kwamba taasisi zimeshafanya utafiti na kuona kuingia kwenye hiyo ununuzi wa mikopo yawezekana kuna risk zake hivyo kama taasisi wakajikita kwenye mikopo mipya ambayo kwao haiwasumbui.
Lakini nikutie tu moyo ndugu yangu,kwa sasa soko ni huria,ukiona hapo hujapapenda fanya window shopping upate sehemu ambayo utaridhika nayo na maisha yanaendelea.
Tukumbuke wako kwenye biashara kwa hiyo wataangalia ni ipi inawafaa kwa mazingira yao.
 
Kwasasa CRDB wananunua. Sjajua kwa hao wengine
 


Mkuu wacha kupotosha NMB wana nunua, tembele atawi la karibu yako ukauze deni lako na upate mkopo.CC: NMB Tanzania
 
nahisi sabab wao wana wateja wengi so wanaringa tofaiti na taasisi ambazo hazina wateja

na pia wanakwepa risk za wafanyakazi wengi wanakopa hela nyingi kisha wanaacha kazi.. na kuiachia benk mikopo chefu chefu
Wakati mwingine MTU, akiwa na mikopo mingi ufanyaji wake wa kazi unakuwa mdogo
 
Tatizo ni riba wewe, bank zinatofautiana viwango vya riba kama hukufahamu fahamu sasa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…