Benz C Class na E Class

Watu engine bana! wanajifanya hawaijui bongo!.....machejo tu. Bongo kununua gari mpya mpaka uwe FISADI! Acha tujinafasi na mayuzdi zetu...teh...teh! ngoma ya mwaka 2000 mpya kabisa bongo, ndiyo ni hatari kwa mazingira na usalama, lakn viwanda vilivyopo Japa ni HATARI zaidi kwa afya na usalama. Mtu anahitaji gari kwa ajili ya kuendea kazini, uwezo wake ndy huo kwa nini akope Mapesa kibao?
YA NINI UTUMBO UTUPWE WAKATI WENYEWE TWALIA NDIZI!

Karaghabaho na utozi wenu!
 


Acha mbwembwe kimweri, kila mtu anajikuna anapofikia!!

Unazungumzia mitumba kuja africa?? Mbona hata ulaya na marekani kwenyewe kuna watu wananunua magari mitumba???

Kila mtu anajikuna anapofikia!! Huwezi kugombania daladala huku unaki dola 10k chako kiko ndani kinazagaa zagaa!!

Huku bondo watu wananunua chupi na blauzia za mitumba, ije kuwa gari???

We mwenyewe kuwa kwako ughaibuni kote bado una gari ya mtumba!!!

Watz wenzangu endeleeni tu kununua hizo BMW na Benz za US$ 800 (FOB DSM Port)!!

Kila mtu anajikuna mpaka pale mkono unapofikia!!
 
Ni kweli ulichikisema mkuu.nimewahi kuwa nazo hizo E na c,ni gari nzuri sana na huwa hazina matatizo ila ujenge mazoea ya kufanya service.kuhusu vifaa vinapatikana pale sinza kuna jamaa anayo garage kwa ajili ya mabenzi tu,ni hela yako kama unataka used au nahitaji vifaa vipya.
 

Kwani haya mabenz yanamilikiwa na watu wanaoishi Dar tu, wapeni data za sehemu za kufanyia service na kupata spare parts na ndugu zetu wa mikoani. Jamaa zetu pale Kasulu, Isaka na Namtumbo watakua wanahitaji kujua hizo sehemu ili angalau wakaservice ma Benz yao!!
 

umesema kweli mkulu!!!
sisi wa tunduru tuambieni spare zinapatikanaje?......natania jamani, huku vijijini saluni utaiendeshea wapi? huku tunaendesha patrol, prado, landrover na isuzu tuu....teh! teh! Hata spea tunaagiza kwenye mabasi ya SuperNajimunisa, Akamba, SuperFeo, Mohamed Trans na Sumry!!!! teh teh! inafika kwa bei mara tatu ya bei yake ya dukani!
SHAMBANI RAHA TUPU, SIJI MJINI NG'O!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…