Benzema aitwa tena Ufaransa

tc_edo

Senior Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
123
Reaction score
98
Haikuwa kipindi chenye furaha sana kwa Karim Benzema, mchezaji wa Real Madrid na raia wa Ufaransa baada ya kukosa kuitumikia timu yake ya taifa kwa miaka 5 kwa tuhuma za kuhusika kumlaghai mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena kwa video ya mapenzi miaka mitano iliyopita.

Kocha Didier Deschamps mwaka huu kaamua kumuita tena nahodha huyo mwenye magoli 29 katika michuano yote msimu huu (2020/2021) baada ya kuongea nae kirefu zaid. Karim Benzema ataitumikia timu yake ya taifa katika michuano ya Ulaya (EURO) itakayo anza mwezi Juni mwaka 2021.

Wafautao ni wachezaji waliopata nafasi kuitumikia Ufaransa katika michuano ya Euro 2021.

Kipa- Hugo Loris, Steve Mandanda, Mike Maignan

Beki wa kati - Raphael Varane, Kurt Zouma, Presnel Kimpembe, Jules Kounde, Clement Lenglet

Beki wa pembeni Kulia - Benjamin Pavard, Leo Dubois

Beki wa pembeni kushoto - Lucas Hernandez, Lucas Digne

Viungo - Adrien Rabbiot, N'gole Kante, Paul Pogba, Corentin Tolisso, Moussa Sissoko

Winga wa kulia - Antoine Griezmann, Ousmane Dembele, Kingsley Coman

Winga wa kushoto - Kylian Mbappe, Marcus Thuram, Thomas Lemar

Striker - Karim Benzema, Oliver Giroud, Ben Yedder. View attachment 1790231
 
kwa tuhuma za kuhusika kumlaghai mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena kwa video ya mapenzi miaka mitano iliyopita.

Kwa hiyo Benzema ni gay, alitumia mkanda wa mapenzi kumtongoza mchezaji mwenzake.

Ungecheki online dictionary ingekwambia maana ya blackmail, acha uvivu.

Benzema pamoja na wenzake watatu walijaribu kumtoa hela mchezaji mwenzake wa Taifa wa Ufaransa kwa kumtishia kusambaza mkanda wake wa video ya matusi. Benzema ndie aliyetumwa kuongea nae moja kwa moja

Kesi ya Benzima itaanza kuunguruma mahakamani katikati ya michuano ya Euro 2020 itayoanza June 2021.
 
France ndo chama langu.
Kwa anaejua anijulishe,hivi huyu Marcus Thuram ni mtoto wa beki wa zamani wa France Lilian Thuram?
 
Hivi huyu golikipa MANDANDA bado yupo tu? Si kacheza na kina Bernad Lama
 
Hivi huyu golikipa MANDANDA bado yupo tu? Si kacheza na kina Bernad Lama

Huyu Mandanda yawezekana kuwa ndio mkuu wa kamati ya ufundi wa timu.
Haiwezekani kipa bomu kama huyu halafu daima asikosekane kwenye kikosi cha timu kubwa kama France
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…