Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Akiwa katika hali ya kuzimia na kupoteza fahamu Beria atamsema vibaya kufikia hadi kumtema mate na anapoonyesha dalili za kuzinduka atamshika mkono na kuubusu kuonyesha mapenzi akihofia labda huenda Stalin akanyanyukia kutoka yale maradhi yanayomsibu.
Haya anayafanya kwenye chumba cha Stalin wakati kalalia kitanda chake cha umauti.
Beria mtu mnafiki na msaliti.
Katika kitabu hiki na alipoeleza haya kuhusu Beria, Stalin akasema kuwa Beria alijiunga na chama kwa maslahi yake binafsi si kwa mapenzi ya nchi yake.
Ukiwa umejaaliwa kusoma vitabu vingi kuna kitu kinajengeka ndani ya ubongo wako mfano wa mafaili madogo madogo yenye taarifa ndogo ndogo ambazo ukitaka unaweza kuziunganisha ukapata vitu katika hizo faili vinavyoeleza jambo au tukio lililo mbele yako.
Ajabu yake ni kuwa wala huhitaji kufikiri sana kwani hizo faili zunajifungua zenyewe na kujiunganisha zenyewe.
Kichwa cha habari ni Beria, msaliti wa Joseph Stalin utamsoma katika kitabu cha Khrushchev, ''Khrushchev Remembers,' na Brutus yumo katika ''Julius Caesar,'' mchezo maarufu wa William Shakespeare.
''Et tu, Brutus?''
Maana ya maneno haya ni, ''Hata wewe Brutus?''
Maneno haya aliyasema Caesar alipomuona Brutus anamkabili kumshindilia upanga wa kummaliza pale maadui zake wala njama walipokuwa wamemzunguka wamempiga mapanga na Brutus ambae hakumtegemea akidhani ni rafiki na yeye yumo katika kundi la kumuua.
Hawa ndiyo watu wa siasa.
Lakini nani huyu Beria?
Huyu Beria alikuwa Mkuu wa Idara ya Usalama ya Urusi.
Brutus alikuwa jenerali katika jeshi la Roma.
Ukiwaangalia wote Beria na Brutus walikuwa watu wakubwa katika serikali lakini wote waliwasaliti viongozi wao.
Hawa ndiyo watu wa siasa.
Beria mwisho wake aliuliwa na viongozi wenzake akina Khrushchev baada ya yeye kuliwa njama kwa hofu kuwa akishika uongozi wa nchi hatabakisha mtu.
Brutus alijiua.
Ukifuatilia siasa katika nchi zetu za Afrika wakati mwingine ni kama vile unaangalia ''Soap Opera,'' yaani tamthliya isiyokuwa na mwisho.
Faili nyingi zitakuwa zinakufungukia.
Unajiambia huyu mfano wake kama Beria, huyu kama Brutus, huyu Lancelot Gabbo mchekeshaji katika ''Merchant of Venice.''
Raha ya haya yote ni kuwa unapata burudani ya bure, ''zero cost,'' mwezi mzima na ikisha hii inaingia hii gharama yako vocha ya simu yako uingie katika mitandao ya kijamii.
Lakini raha anapata yule ambae akili yake imehifadhi mafaili yenye taarifa tofauti, tofauti akaziunganisha akapata kitu kizima na kingine mfano wa ''series,'' iliyopo mtandanoni.
Lakini raha anapata yule ambae akili yake imehifadhi mafaili yenye taarifa tofauti, tofauti akaziunganisha anapata kitu kizima na kingine mfano wa ''series,'' iliyopo mtandanoni.
Siku moja nimeswali Msikiti wa Badawy ulioko Soko Mjinga Kisutu.
Jirani na msikiti huu ni Viwanja Vya Mnazi Mmoja Augustino Mrema anaunguruma wakati wa Uchaguzi Mkuu 1995.
Kelele na vifijo kutoka Mnazi Mmoja vinaingia hadi ndani msikitini.
Tumemaliza kuswali watu wanatoka nje wanachukua viatu haraka haraka kwenda kumsikiliza Mrema.
Mimi na mwenzangu tumebaki nje ya msikiti na Imam wetu Shariff Adnan.
Yeye kaegemea ukuta na ukimtazama ni kama mtu hayupo hata pale tulipo yuko dunia nyingine kabisa.
Nikamwambia mwenzangu, ''Unamuona Shariff hata kusikiliza mkutano hapo alipo hasikilizi namuona yuko mbali sana.''
Mwenzangu akanijibu, ''Shariff huyo mwanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir yeye kayaona yote haya miaka mingi nyuma na hata haya ya leo ya Mrema keshajua yataishia wapi.''
Kasema mwenye kusema, ''If you have patience you will see the end of everything.''
Ukiwa na subra utaona mwisho wa kila kitu.