Bernard Arnault, mmiliki wa kampuni ya LVMH, ammpiku utajiri Mark Zuckerberg, na kuwa mtu wa tatu kwa utajiri Duniani.

Bernard Arnault, mmiliki wa kampuni ya LVMH, ammpiku utajiri Mark Zuckerberg, na kuwa mtu wa tatu kwa utajiri Duniani.

Last Seen

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
229
Reaction score
566
Bernard Arnault, mmiliki wa kampuni ya LVMH, amempita utajiri mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg, na kuwa mtu wa tatu kwa utajiri zaidi duniani. Hii inatokana na ongezeko la thamani za hisa za LVMH, kampuni inayomiliki bidhaa maarufu kama Louis Vuitton, Moët & Chandon, na Hennessy.

Utajiri wa Arnault umefikia dola bilioni 155, akimzidi Zuckerberg ambaye utajiri wake ni dola bilioni 150. Hii inamfanya Arnault kuwa nyuma ya Elon Musk na Jeff Bezos pekee katika orodha ya matajiri wakubwa duniani.

Kampuni hii inamiliki brands za nguo, vinywaji, na bidhaa za urembo. Ongezeko la thamani ya hisa za LVMH limechochewa na mauzo mazuri ya bidhaa zake, hasa katika masoko ya Asia na Marekani.

Bernard Arnault, ambaye ni raia wa Ufaransa, ameiongoza kampuni ya LVMH kwa zaidi ya miongo mitatu. Uongozi wake umeifanya kampuni hiyo kuwa moja ya kampuni zenye mafanikio makubwa zaidi duniani.

Mark Zuckerberg, ambaye alianzisha Facebook akiwa na umri wa miaka 19, amekuwa akipanda na kushuka kutokana na ushindani mkali kutoka mitandao mingine ya kijamii.
 

Attachments

  • ar.jpeg
    ar.jpeg
    19 KB · Views: 10
Daah, ila sasa tatizo age yake, Mack Zuckerberg kwa age yake bado ana advantage.., akifika umri wa hao wengine vibabu, atakuwa hashikiki
 
Back
Top Bottom