Uchaguzi 2020 Bernard Membe achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Afadhali na yeye amepata nafasi ya kupokea kibegi hicho, huenda itamsaidia kuondoa msononeko wa akili. Lowasa alipata kubeba kibegi hicho kutokea CHADEMA na kuahidi mafuriko ambayo hayakutokea lakini sasa hivi hana msononeko tena. Baada ya uchaguzi, nadhani hatakuwa na msononeko wala kelele tena.
 
zitto karamba joker sisi red bregedia tunaumia sana katuzidi ujanja bwana zuberi
 
Wanajamvi.
Kwanza tuweke sawa vitu.
Hapo awali kugombea uraisi kwa upinzani hakujawahi kuwa kitu rahisi au chepesi sana,huwa ni maamuzi mazito ya kujikana nafsi yako na kubeba msalaba wako mwenyewe.

Wepesi huu ulianza kujengeka mwaka 2015 baada ya sisi wenyewe kujiaminisha kwamba hatuwezi kuing'oa MCC wenyewe ila mpaka MCC "wenyewe" waje watusaidie kuing'oa (wajing'oe wenyewe).

Inafikirisha sana leo mtu kuweza kuongelea uamuzi wake wa kuing'oa MCC kwa aya mbili tu,huku kiu yake ikiwa kuungana wapinzani na wamsimamishe yeye.

Kwamba "kaombwa" pale Mlimani city,kapanda Range rover yake,kurudi kwake "ushuani" kaenda kutafakari na mkewe usiku kucha halafu asubuhi amekubali kubeba hiyo dhamana ya machozi,jasho na damu ya kuing'oa MCC yenye umri wa kikongwe madarakani. Aisee

Kwa upande mwingine: TL (simpigii chapuo) mwisho wa mwezi anakuja. Atadakwa fasta kwa kisingizio cha kesi za kuungwa ungwa. Usiku huo wa kuja TL "Elites" hawatalala na atadakwa hapo hapo uwanjani.
Maskini kaamua kujikana TL.Hayupo upande wao,hashiriki meza yao,hana urafiki nao na shilingi yao kaikataa. Usiku huo "wa kudakwa kwa TL,kwa kuwa ni mwisho wa mwezi "jasusi mbobezi" na "Kijana wa Mwandiga" wao watakuwa "ushuani" Masaki au Oysterbay wamelala na wake zao,wana amani tele moyoni huku wakisubiri kutimiza mpango wao oktoba 2020 na wapewe chao.

Mkutano wao haukuvamiwa,kubanwa kibali wala kuingiliwa na makamanda hapo Mlimani city. Walikula na kunywa huku wakigonga glasi na wala hela ya kampeni kwao haikuwa ajenda. Chama ambacho hakipo katika paycheck ya ruzuku hakiumizi kichwa kumzungusha Mgombea wake wa uraisi nchi kubwa kama Tanzania! Hela anakuja nayo "Mbobezi" ha ha ha.

Mpango wa siku nyingi
"Elites" kama alivyoada wao mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa kuandaa uchaguzi mwingine.

Mbobezi ni trap na lengo lao ni kupunguza kura za CDM na kuitoa katika "key opposition",misheni ya muda mrefu sana na mratibu ni ZK.

Kama ilivyokuwa 2015,imepangwa chama dola washindane wao kwa wao huku tukipiga kelele na kuwashangilia.

Mbobezi akimaliza uchaguzi huu,MCC watamrudishia uanachama "kimasihara" kama walivyomfukuza "kimasihara".

ZK mpango wake ni kugombea 2025 ambapo atakuwa ametimiza lengo la kuimaliza CDM kama chama kikuu cha upinzani bara na CUF kufutika visiwani.

ZK anahitaji ruzuku bara na visiwani kuelekea 2025.

Mbobezi yeye yupo kazini,"Elites" walitengeneza na kwa makusudi amepewa yeye atakeleze huo "Mpango".

Kila kitu atapata Mbobezi,mabango,bendera,chopa,posho,magari na atafika kila kijiji hapa bongo kujinadi. Kwa siku 60 za kampeni hawatapungukiwa hata mafuta achilia mbali mabango. Kama 2015 kwa EL vijana walitundika bendera za CDM "Made-in-China" kwenye miti.

Wacha picha iendelee bwana.

Wasaalam

"Ukiwa na subra,utaona mwisho wa kila kitu.

"Upepo ukivuma sana,uchi wa kuku huonekana"
 
Ccm Mwisho Wenu Umekaribia...


Nchi Yetu Sote...


Na Mwaka Huu Mtaelewa kwa nini Kaka Man Aliimba Kama Noma na Iwe Noma.
 
Ccm Mwisho Wenu Umekaribia...


Nchi Yetu Sote...


Na Mwaka Huu Mtaelewa kwa nini Kaka Man Aliimba Kama Noma na Iwe Noma.

Alisina.
Unaamini CCM ndio mwisho wao mwaka huu? Kama ndivyo,basi tujipe subra.
 
The second incidence, the repeated blunder done with our juvinile opposition parties
 
Hi kuna tofauti gani kati ya kugombea "URAIS" na kugombea "KITI CHA RAIS"?








=============================================================================







 
Kipindi chake Tanzania iliyumba kimahusiano na Rwanda,Malawi na ilifanya uvamizi haramu huko comoro!
 
Eeenh mkuu 'Alpha 13'.

Wewe ungekuwa mwanafunzi wangu unapata yai hapo hapo!

Unatoka kwenye mada unapiga zako kusikohusika kabisa na mada.
 
Eeenh mkuu 'Alpha 13'.

Wewe ungekuwa mwanafunzi wangu unapata yai hapo hapo!

Unatoka kwenye mada unapiga zako kusikohusika kabisa na mada.
Naomba unisahihishe mwalimu, nimekosea wapi?
 
Naomba unisahihishe mwalimu, nimekosea wapi?
Usimfanye mwalimu akuone wewe hufundishiki.

Huwezi kusoma majibizano yalipoanzia ukajua umetoka nje ya somo? Sasa unataka ulishwe kabisa?
 
Usimfanye mwalimu akuone wewe hufundishiki.

Huwezi kusoma majibizano yalipoanzia ukajua umetoka nje ya somo? Sasa unataka ulishwe kabisa?
Some lilikua wananchi vs sheria. Mwenzangu alitegemea niwatetee wananchi, nilipochangua upande wa sheria akajanikosoa "wananchi ndio watunga sheria kupitia wawakilishi". Nikamjibu sheria zinatungwa kutoka kwenye morals "elimu ya mema na mabaya" ambayo ilikuepo kabla ya wananchi wote tuliopo sasa.

Ili kupunguza mvutano nikaenda hatua moja mbele kuonyesha chimbuko la elimu hii ya mema na mabaya mizizi yake ipo kwa Mungu.

Point yangu ni hii; sheria ndio muongozo, viongozi inawapasa wazisimamie pia wawe mfano kwa kuzitii ili wananchi wote tuzifuate.
 
Mtatunga sana hizi hadithi zisizo na miguu wala vichwa.

Tundu Lissu, atakuja hapa kama shujaa anayekuja kuikomboa nchi toka utumwani.

Hakuna shujaa aliyeogopa kujitoa maisha yake kuikomboa nchi yake.

Kuwekwa ndani sio mwisho wa mapambano, ni mwanzo tu wa mapambano hayo.

Kwa hiyo msiitumie vitisho vya Lissu kuwekwa ndani kama kinga yenu ya kuendelea kuwakandamiza wananchi wa taifa hili. Lissu ni sehemu tu ya mapambano ambayo hamuwezi kuyazima sasa.
 
Basi ngoja niseme sipo kwenye 'mood' wa kuku'engage' kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…