Msukuma Original
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 928
- 3,330
Membe amuunge mkono Lisu. ACT ni chama kichanga sana. Haiwezekani mgombea wa urais atoke ATC. CHADEMA ina wanachama wengi sana haiwezekani mgombea atoke kwenye chama kisichokuwa na wanachama wengi.
Ujio wa Membe hautakuwa na impact kubwa sana kwenye upinzani. Membe anajulikana ukanda wa kusini tu. Tanzania ni kubwa sana, watu watakaokuja na Membe upinzani ni asilimia ndogo sana ya wapiga kura wa Tanzania nzima.
CHADEMA msifanye kosa mkamuunga mkono mpinzani yoyote wa nafasi ya urais zaidi ya Lisu. Upinzani mkichukua nchi tafadhalini myaendeleze yote mazuri anayoyafanya Magufuli. Miradi yote aliyoianzisha Magufuli ambayo haijakamilika mkaikamilishe. Hizi ni hela za watanzania. Haiwezekani kila rais anayeingia anakuja na mambo yake mapya na kuyatelekeza ya mtangulizi wake.
Watanzania walio wengi wanaifurahia miradi inayofanywa na Magufuli. Hakuna asiyefurahia kuona miradi mikubwa kama hii inatekelezwa. Kwenye kampeni zenu nendeni mkawaambie wananchi kuwa hakuna hela ya watanzania itakayopotea kwenye hii miradi aliyoianzisha Magufuli, mnaenda kuikamilisha pale alipoishia.
Mkimsimamisha Membe mnaenda kushindwa vibaya sana. Membe hajulikani kwingine kote isipokuwa ukanda wa kusini na kwenye mitandao ya kijamii. Wapiga kura wengi hawapo kwenye mitandao ya kijamii.
Binafsi natamani Magufuli aendelee kutawala ili akamilishe miradi aliyoianzisha.