Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Mimi sio kachero, nimegombea kuchukua kiti cha urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Mimi sio kachero, nimegombea kuchukua kiti cha urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Mngurimi

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
819
Reaction score
790
Nimetoka kusikiliza mahojiano ya mgombea urais wa JMT kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo muda mfupi uliopita kwenye kituo cha DW. Mtangazaji katupa maswali ambayo nilikuwa nikitamani sana siku moja kusikia BM mwenyewe akiyatolea ufafanuzi licha ya kusikia juu juu tu.

Moja kati ya swali ambalo kaulizwa ni kuhusu yeye kuhusishwa sana na ukachero na yawezekana kabisa akawa amepandikizwa na chama tawala ili kuuwa nguvu ya upinzani kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Bernard Kamillius Membe ameweka wazi kabisa kuwa, yeye ameamua mwenyewe kugombea na kuwania nafasi ya urais wa JMT wala sio pandikizi kama fikra za baadhi ya watu zinavyodai. "Kama ni kutumwa, unadhani nitakuwa nimetumwa na nani? Kwa lengo lipi? Au kwa kupata cheo kipi, ambacho kufumba na kufumbua unaweza kujikuta umetumbuliwa?", amesema Membe.

Mbali na hayo yote, Ndugu Bernard Kamillius Membe amesema kitendo cha yeye kuja ACT-Wazalendo ni kwa sababu ya kuchoshwa na mambo yalivyokuwa yakifanyika upande wa pili na ndiyo maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya wabunge waliomfuata na wala hawakwenda kwenye vyama vingine.

Source: DW
 
Nimetoka kusikiliza mahojiano ya mgombea urais wa JMT kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo muda mfupi uliopita kwenye kituo cha DW. Mtangazaji katupa maswali ambayo nilikuwa nikitamani sana siku moja kusikia BM mwenyewe akiyayolea ufafanuzi.

Moja kati ya swali ambalo kaulizwa ni kuhusu yeye kuhusishwa sana na ukachero na yawezekana kabisa akawa amepandikizwa na chama tawala ila kuua nguvu ya upinzani kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Bernard Kamillius Membe ameweka wazi kabisa kuwa, yeye ameamua mwenyewe kabisa kugombea na kuwania nafasi ya urais wa JMT. "Kama ni kutumwa, unadhani nitakuwa nimetumwa na nani? Kwa lengo lipi? Au kwa kupata cheo kipi, ambacho kufumba na kufumbua unaweza kujikuta umetumbuliwa?", amesema Membe.

Mbali na hayo yote, Ndugu Bernard Kamillius Membe amesema kitendo cha yeye kuja ACT-Wazalendo ni kwa sababu ya kuchoshwa na mambo yalivyokuwa yakifanyika upande wa pili na ndiyo maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya wabunge waliomfuata na wala hawakwenda kwenye vyama vingine.

Source: DW
Mgombea wetu Bernard Membe haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa (Hashim Rungwe) anaonekana.
 
Membe jitulize tuu, ulianza safari na mguu mbaya. Kila Bwana ana Bwana wake. Kwasasa #Ni Yeye Lissu 2020.

Ama huoni Magufuli anavyohenyeshwa hadi anataka kutapika ulimi?
 
Hawezi kukubali kua ni mamluki wa ccm ila uhalisia unajionesha na ndio maana zitto kamtema
 
Mh.Rais Mtarajiwa Benard Membe...

Anakwenda Kushinda Kwa Kishindo Kikuu...

Dakika za lala salama ni faida kwa Mtarajiwa Membe....

Ombi langu Kwake...

1.Asifute Makao Makuu Na Ikulu Kuwa Dodoma.
2.Asisitishe Mradi Bora Kabisa Wa Bwawa La Umeme pale Rufiji.
3.Asisitishe Ujenzi Wa Reli Ya Kisasa SGR.

Kila la heri kwa Rais Wetu Mtarajiwa BC Membe Mzee Wa Mtama,Mtunduizi Wa Dakika ya 89.


Muuza Al Kasus,Kwa Mtogole.
 
Ccm walicheza vibaya sana karata zao hapa,

Wangemtengeneza hata yule jangili ana nguvu mara mia mbili ya maembe.
 
Hahahahahah

Membe kagombana na JPM sio CCM kama ambavyo Lowassa aligombana na Jk sio Ccm

Kweli kabisa, hata Jana nimelisema hilo huku jukwaani. Membe Ana ugomvi binafsi na Magufuli, na ameenda upinzani ili kutingisha kiberiti au kutakatisha nyota, ili apande thamani. Hakuna mwanaccm aliyemalizia ujana wake ndani ya ccm anaweza kuishi nje ya ccm. Sana sana mtu huyo asiporudi ccm kama Lowasa, Sumaye nk, atageuka kuwa kibaraka wa ccm mfano Mrema, Shibuda nk.
 
Back
Top Bottom