Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amefikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, huku maombi ya mawakili wake ya kutaka apelekwe hospitalini kwa matibabu yakikataliwa.
Besigye (68) alionekana mahakamani Ijumaa, Februari 21, 2025, akiwa dhaifu na ameketi kwenye kiti cha magurudumu (wheel chair) baada ya kugoma kula tangu Februari 12 kupinga kuwekwa kwake kizuizini.
Inaripotiwa kuwa Besigye na msaidizi wake, Obed Lutale, walitekwa nyara jijini Nairobi, Kenya, na kurejeshwa kwa nguvu Uganda mnamo Novemba mwaka jana.
Baada ya kurejeshwa, walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi wakikabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na uhaini.
Uamuzi wa Mahakama ya Juu mnamo Januari 31 ulieleza kuwa raia hawawezi kushtakiwa katika mahakama za kijeshi, na hivyo kesi yao kuhamishiwa mahakama ya kiraia.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ilisoma mashtaka mapya ya uhaini na kula njama ya kutenda uhaini dhidi ya Besigye, ikidai kuwa alikuwa akipanga kuiangusha serikali ya Rais Yoweri Museveni.
Hakimu Esther Nyadoi alieleza kuwa mahakama yake haina mamlaka ya kuendelea na shauri hilo, kwani mashtaka hayo yanapaswa kushughulikiwa na mahakama za juu zaidi.
Chanzo: The Citizen