real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Aliyekuwa mgombea urais Dk Kizza Besigye ameshinda kesi yake dhidi ya Shirika la Utangazaji Uganda (UBC) kwa kukataza matangazo yake ya kampeni za mwaka 2011.
Mahakama Kuu chini ya Jaji Margaret Ogulion Jumatatu ilitoa hukumu iliyompa ushindi Dk Besigye na fidia ya Sh80 milioni zikiwa ni gharama na uharibifu baada ya kusikia alililipa shirika hilo la kitaifa Sh21 milioni kwa ajili ya matangazo yake ya kampeni kabla ya uchaguzi wa rais mwaka 2011, lakini wao (UBC) walishindwa kuheshimu makubaliano hayo.
Wakati wa usikilizwaji wa kesi, Besigye alilitaka shirika la UBC kumrejesha Sh21 milioni.
Aliiambia mahakamani kuwa shirika hilo la kitaifa lilichukua fedha zake wakati wa kampeni ya urais wa 2011, lakini kamwe halikutangaza matangazo yake ya kisiasa.
Hilo lilimkasirisha Besigye ambaye pia alisema kesi yake imechukua muda mrefu katika mahakama baada ya kufunguliwa mwaka 2011.
Miongoni mwa yaliyopewa uzito, pia Besigye aliomba UBC izuiwe kufanya ubaguzi wa watu kwa misingi ya itikadi za kisiasa.
Kwa mujibu wa kesi hiyo iliyofunguliwa dhidi ya UBC na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani Edward Musinguzi, kampuni hiyo ya utangazaji ilipokea Sh21 milioni kutoka kwa wakala wa vyombo vya habari wa Besigye, Big Ideas, ili kutangaza mara 200 kampeni zake za urais mwaka 2011, lakini hawakufanya hivyo.
Chanzo: Mwananchi