Besigye, upinzani walaani kuuawa kwa Mbunge Abiriga

sky walker

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
1,160
Reaction score
831
F21FF65B-DFC7-4AB3-B09F-137C985E9617_w1023_r1_s.jpg

Rais wa zamani wa chama cha upinzani cha FDC Uganda, Dr Kizza Besigye na viongozi wengine wa upinzani nchini humo wamelaani mauaji ya Mbunge wa Manispaa ya Arua, Ibrahim Abiriga.

Jeshi la polisi na bunge mapema walisema kuwa Abiriga (wa chama cha NRM) pamoja na mlinzi wake waliuwawa karibu na nyumbani kwake huko Kawanda katika wilaya ya Wakiso jana jioni.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema washambuliaji hao walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki.

Pamoja na kuwa Abiriga alikuwa upande ulioanzisha mjadala juu ya suala lenye utata la ukomo wa umri, viongozi wa upinzani akiwemo Dr Besigye, rais wa chama cha DP Norbert Mao, Erias Lukwago, Dr Abed Bwanika wamejitokeza kulaani mauaji hayo.

Akieleza wasiwasi wake juu ya mauaji haya, Dr Besigye alituma ujumbe wa tweet akielezea tukio hilo kama ni janga na kuongeza kuwa hali ya kutokuwepo usalama Uganda sasa imefikia kiwango cha kumuathiri kila mtu.
 
Aiseee "" Hawa madikteta ...mbona wana roho mbaya hivi "" yaani hao waganda wote wamekubali kufanywa popoma na mtu mmoja tu "" Miaka nenda rudi ""...!!!!!
 
na rwanda "kwa rafiki yetu" the same case.

nikukumbushe tu hawajakubali ila wamelazimika/wamelazimishwa kuwa ktk hiyo hali.

1• kanuni ya kwanza waumize wale viherehhere kiuchimi

(hakuna stakaye enda front line huku akijua mwanae anafukuzwa ada, jengo lake linabomolewa mmoja wa wanafamilia wake hajulikani alipo so wanaku keep bze mpaka unaachana na harakati

2•kanuni ya pili. Poteza wote wanaojifanya wagumu, wabishi na wanasapoti kubwa ndani na nje ya nchi.
(ndio unaona kama hivyo watu kuuawa kupotezwa kutekwa na kufanyiwa vitu vibaya n.k)

3• kanuni ya tatu. Tutumie wingi wetu bungeni na serikalini kupitisha vifungu vinavyo tubeba kimadaraka.

bye
 
Asante kwa Uchambuzi .......inasikitisha sana kwakweli "..... mtu anapigwa risasi kama kuku kisa tu kuipigania democracy
 
He kumbe wewe huwa unakula Kuku waliopigwa risasi!! Makubwa!
 
Alikuwa hapiganii demokrasia, alikuwa anapigania tumbo lake kwani mmoja wao waliokuwa wanapiga debe umri wa kugombea urais uongezwe ili mseven agombee tena
 
hahaha wapi nimesema huwa nakula " kuku waliopigwa risasi mkuu"".... hebu malizia kwanza hiyo balimi yko " kisha hangover ikishaisha ndio uje kuchangia hoja
 
Alikuwa hapiganii demokrasia, alikuwa anapigania tumbo lake kwani mmoja wao waliokuwa wanapiga debe umri wa kugombea urais uongezwe ili mseven agombee tena
Alaaaa kumbe """!!!..... so sad
 
Tanzania, Dodoma kwenye nyumba za serikali na cctv camera zikatolewa haraka kuficha aliyemmiminia Tundu Lissu risasi 38 mchana kweupe.
 
F21FF65B-DFC7-4AB3-B09F-137C985E9617_w1023_r1_s.jpg

Rais wa zamani wa chama cha upinzani cha FDC Uganda, Dr Kizza Besigye na viongozi wengine wa upinzani nchini humo wamelaani mauaji ya Mbunge wa Manispaa ya Arua, Ibrahim Abiriga.

Jeshi la polisi na bunge mapema walisema kuwa Abiriga (wa chama cha NRM) pamoja na mlinzi wake waliuwawa karibu na nyumbani kwake huko Kawanda katika wilaya ya Wakiso jana jioni.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema washambuliaji hao walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki.

Pamoja na kuwa Abiriga alikuwa upande ulioanzisha mjadala juu ya suala lenye utata la ukomo wa umri, viongozi wa upinzani akiwemo Dr Besigye, rais wa chama cha DP Norbert Mao, Erias Lukwago, Dr Abed Bwanika wamejitokeza kulaani mauaji hayo.

Akieleza wasiwasi wake juu ya mauaji haya, Dr Besigye alituma ujumbe wa tweet akielezea tukio hilo kama ni janga na kuongeza kuwa hali ya kutokuwepo usalama Uganda sasa imefikia kiwango cha kumuathiri kila mtu.
Yana Mwisho! Na pia ukibarikiwa,pia vinabarikiwa kizazi cha mjukuu wa vituukuu vyako.na pia ukilaaniwa utalaaaniwa ata kizazi cha kumi cha wajuukuu wa wajukuu zako.hii ni bibilia sio maneno yangu!.So do what you can do,toa waraka,kill them.ila neno la Mungu lipo na litaendelea kuwepo kabla na baada ya PotPot
Cambodian genocide - Wikipedia
Kwa Wakatoliki washawai kuvumilia zaidi ya miaka mia Wazalimu waishe waendelee na life yao! Kama wakatoliki.Akuna kiongozi wa east africa ana miaka 60 ijayo atakuwa hai! Familia yake ,watoto waliotoka katika viuno vyake,mahela yake swiss,au Visiwani sijui wapi! Ayatompeleka mahali salama! Na pia ataonja mziki wa Mungu kama Mugabe na viongozi MFALA Wengine wa dunia hii!
 
Back
Top Bottom