Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 950
- 1,672
Dr King (M.L.King Jr) alishawahi nukuliwa akisema “ Not everyone can be FAMOUS , but everyone can be GREAT. Japo hotuba yake ilikuwa yenye mlengo wa kisiasa, lakini kupitia nukuu hii alikuwa anajaribu kutonesha kuwa kuna utofauti kati ya Umaarufu(Fame) na ubora(Greatness).
Kwa lugha nyepesi, unaweza kuwa maarufu lakini usiwe bora, pia unaweza kuwa bora lakini usiwe maarufu.
Kuungana na kile alichokisema Dr King, leo nimewaletea series ambazo ni bora lakini sio maarufu. Hapa namaanisha zimetazamwa na watu wachache, na wakati wengine kuamini kuwa kutokana na ubora wa hizo series basi hazijapata heshima zinazostahili.
Kama tayari umeziona utaungana kwa kupinga au ku-support ili wengine wapate kuzitazama.
The OA
Jaribu kupita kwenye mitandano kadhaa ambayo wana-discuss masuala ya filamu , basi kila penye The OA utakutana na hash tag ya bring back the OA.
Ni filamu ambayo Netflix waliacha kuendelea kuizalisha wakidai imekosa watazamaji. Lakini kwa sasa inaongeza watazamaji kila kukicha baada ya kila atakayetazama anakuja na positive feedback.
Ni series bora sana, japo imejaribu kugusa baadhi ya mambo makubwa sana na yenye kufikirika kama vile nadharia ya multiverse, uwezekano wa kusafiri kutoka dimension moja kwenda nyingine, na issue ya NDE(Near Death Experience), huku iki-question mambo mengi sana, nahisi hata Netflix wakaona hawa vijana wanataka kunigombanisha na Muumba(Mungu), wakaisitisha, haha(Jokes).
Ila hata kama wamesitisha bado ni nzuri na unaweza tazama bila kuathirika na ushitushwaji wake.Ni Series yenye Season 2 tu.
Foundation
Ukitoa The Expanse(ambayo pia ni underrated). Foundation ndio tafsiri kamili ya Game of thrones on space.
Hapa nitatoa lawama na pongezi kwa Apple TV, hawa jamaa wana series bora sana hasa Sci-Fi ila hawazitangazi, promo yake ni zero. Ila Foundation ni series bora sana yenye season 2 hadi sasa, ila bado inaendelea.
1899
Hii pia ni zao la Netflix. Ukitaja hii series basi huwataacha kuitaja series ya Dark, sio sababu sinafanana ila mtayarishaji(creator) ni mmoja. Ni moja ya series bora sana, japo inaanza taaratibu hadi pale utakapoelewa kinachoendelea.
Bila ku-spoil, basi concept kubwa ni simulation, pia ime-question mambo mengi sana kuhusu brain/mind, perception and reality. Hii radha utaipata katika season 1 pekee.
Mind Hunter
Kitu pekee na uhakika baada ya kumaliza hii series itakomaza uelewa wako kuhusu malezi, mazingira na mchango wake katika ukuaji wa binadamu.
Ni series iliyojaribu kwenda tofauti kidogo na njia ya kawaida katika suala wa upelelezi. Hii imejikita katika kutambua tabia, saikolojia ili kutambua kwanini watu wanafanya kile wanachokifanya mfano Ulawiti, mauaji na unyama mwingine. Series imeonesha wahalifu wengi wamepitia mazingira au malezi fulani ambayo yamechangia kufanya kile kinachofanyika, pia wamekuwa na tabia zinazofanana.
Nimeona ni kweli, simaanishi naunga mkono kile kinachofanyika bali naelewa kwanini wanafanya.(I do not condone, but I understand). Kama hujaitazama, nenda katazame naamini kwa asilimia kubwa utakubaliana na mimi.
Kama ilivyo The OA watu wanapambana Netflix waendelee kuaizalisha, hadi sasa ni season 2 zimekamilika.
Devs
Hii V katika Devs kwa kirumi ni tano si ndio? Na wakati tunasoma irabu naamisha a, e, i, o, U-ni irabu ya tano, kwa maana hiyo DeVs itakua Deus.
Deus ni neno kilatini linalomaanisha God, hivyo basi kuna jamaa alitaka ku-play God katika hii series.Japo tafsiri hii alisema alikua anatania, ila alikuwa ana maanisha. Na mimi nasema natania, ila ni series nzuri bora sana ambayo imeelezea vizuri kuhusu Cause and Effect, prediction, uwezo wa kuvisist past, pia kutabiri the future.
Hii ni season moja pekee, lakini bado imeacha theories nyingi sana kwetu watazamaji.
Uzi umekua mrefu sana, kwa leo naishia hapa. Nitaendelea kutaja nyingine katika reply.
Zipi series umezitama ukaona ni bora lakini sio maarufu au hazipewi heshima yake? Tupe list yako sote tuzitazame.