Best Hip-Hop MC's of all time Bongo (Top five)

mwanazuoni mgeni

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
1,944
Reaction score
1,726
G.morning everyone,
Me ni big fan wa hip-hop ya bongo, na katika research nlioifanya hii ndo list yangu ya MA mc bora wa muda wote waliowahi kutokea hapa Tanzania

1) Professor J,
Huyu jamaa anabaki kuwa no 1 kwa muda wote kutokana na uwezo wake binafsi wa Utunzi wa mashairi na uwezo wa kuandika na kusimamia kwenye Mada anayoielezea tofauti na MA mc wengine Ambao Unakuta jina LA nyimbo na maudhui ya nyimbo yanalandana.

Pia, ni MC pekee mwenye nyimbo nyingi Kali zilizogusa mashabiki wa kila Aina na ni moja ya inspirations kwa new upcoming hip-hop artists. Naweza kumuita God father wa bongo, ktk industry ya music.

2) Albert Mangwea & J. Moe
Hawa jamaa kwangu wanashika no 2 kwa pa1 coz wana uwezo ambao almost unalingana, ukiangalia nyimbo km kimya kimya, kimafia.

Kwaliofanya colabo Wote utagundua uwezo wao n km unafanana, achilia mbal uwezo wa ngwair kwenye free Style.. Na Utunzi wa j.moe akiwa anaelezea story. Wanabaki kuwa best rappers wa muda wote.

3) Chidibenz
Huyu mfalme wa Ilala ni mc hatari Sana,ana vocal na michano mikali sana na pia ana uwezo Mkubwa sana kwenye performance, wengi mnakumbuka enzi zake kwenye kila collabo alikua anakimbiza, Huyu km angepata manager mzur, na angepunguza kiburi jamaa Angekua Mbal sana, kwa Mimi nampa no 3 kwa ubora wake.

4) Langa & Fid Q
Hawa jamaa kwa pa1 nawapa nafasi ya nne, Fid q anauwezo Mkubwa wa kuandika vitu ambavyo viko deep sana na km n mtu unayesikiliza juu juu pengine unaweza usione Au usielewe kabisa ubora wake, Langa alikua na uwezo Mkubwa sana wa ku spit kingereza na kiswahili Hakua na mistari konde Ila alikua anaandika vitu deep sana.

Kwa mtazamo wangu Langa na fid q wanauwezo unaofanana tofauti n kuwa Langa mpaka anatutoka Hakuwa na project nyingi lakini ukisikiliza nyimbo zake utatambua uwezo wake, my favorite line ya Huyu jamaa ni (hawanichekei usoni kisogoni wananisema wanatafuta mabaya wanajifanya Hawaoni mema).

5) Nikki Mbishi (Baba Malcom)
Huyu jamaa ni mkali sana kwenye uandishi na flow anauwezo Mkubwa wa ku free style, ana punch za maana na ngoma ambazo n classic, changamoto nnayoiona kwa Huyu jamaa ni ana km kiburi flan Hv ana attitudes za ajabu ajabu km kudis wanasanii wenzake na ujuaji mwingi.. Ila ni mc hatar sana

Apart from hao top five pia wapo Mc's wengine wakali km stereo, one the incredible, Godzilla, p the mc country boy, na wengine wanaofanya vizuri
 
My top 5

1. Prof J
2. Fid Q
3. SoloThang/JayMo/MwanaFA/Afande
4. Ngwea/Chid Benz
5. Joh Makini
Exactly umeipangilia vilivyo, list umeitendea haki, Atakayekupinga bas ni mchawi au ana lake jambo...nipo hapa naskiliza Ngoma ya prof jay "kikao cha dharula" ikinogeshwa vizur na mdundo mzito wa P-Funk majani
 
1. Fid Q
2. Ngwair
3. Prof J
4. Joh Makini
5. Sugu
6. Jay mo
7. Mbishi na incredible
7. Stamina na Roma
8. Msodoki
9. Nash Mc
10. Dizasta
Itifaki imezingatiwa
Sababu zilizozingatiwa
1. Ukubwa wa maudhui
2. Nafasi yao katika kuikuza hiphop ya kiswahili (bongo hip hop)
3. Ubunifu (upekee wao kifasihi)
 
Tajeni weeee list zenu
Mi huwa namuelewa sana MwanaFalsa aka FA
Bila kuwasahau wafuatao
Ngwea
Prof J
Fid Q
Nature na Babu wa enzi hizo
 
1.Prof Jay
2.Chid Benz
3.Fid q
4.Mangair
5.Jay MO
6.Mwana Fa
7.Solo Thangs
8.Inspector Haroun
9.Afande Sele/Ay
10.One/Niki Mbishi
 
Upcoming

Dizasta vinna

Nala mzalendo

Boshoo ninja

Kinya wa mistari

Maarifa (big thinker)


Bando mc
 
mwanazuoni mgeni,
Sikubaliani na wewe kumuweka Fid Q kwenye level moja na Langa kwa sababu
1. Mistari ya langa ilikuwa imebase kwenye kujisifia wakati Fid anagusa kotekote.
2. Flow ya langa ilikuwa haibadiliki wakati Fid inabadilika
3. Idadi ya ngoma walizonazo na hitsongs Fid anaongoza wakati Langa anasubiri na hii kabla hajafa
4. Fid naye alikuwa anaweza kuflow kwa kiingereza
5. Fid anaweza kuelezea story kwenye flow

Conclusion.
Kumfananisha Fid na Langa nikumkosea heshima Bongo hiphop Icon wetu.
 
Na Chidbenz kuwa juu ya Nikki mbishi jaribu kufanya tathmini tena may be umefanya conclusion ukiwa umebase kwenye upendo ila tukiangalia facts Chidbenz adeserve kuwa juu ya Nikki mbishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…