ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Hivi kazi ya "Best Man" na "Matron" katika harusi ni nini hasa?.
Katika miaka ya hivi karibuni kameibuka ka mtindo kwa wasimamizi wa harusi ("Best Man" na "Matron") kutumika tu siku ya shughuli kama mapambo na pengine huwa ni seti mbili tofauti, kama kandambili za mguu moja. Utakuta Bwana kivyake na bibi kinyake (bestman hamfahamu bibi harusi wala matron hajui chochote kuhusu Bwana harusi).
Katika harusi nyingine utakuta maharusi wanahangaika kutafuta watu wa "kumechi" nao kwa maumbo, mwonekano na vipimo na pengine hata kwenda kumkodisha "matron au bestman" wasiemfahamu ilimradi tu wapate kupendeza siku ya harusi....na siku ikiwadia unakuta Bestman au Matron kazi yake ni kufuta jasho tu la bwana au bibi harusi.
Hivi hakuna Hadidu za Rejea (Terms of Reference) za "Best Man" na "Matron"???