Best Photocopy Machines and Scanners

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
8,447
Reaction score
19,425
1: HP
2: Epson
3: Canon
4: Dell
5: Mo Dewji
Hii namba tano tujikumbushe
(I) Azam Energy- Mo energy
(II) Azam Ukwaju- Mo Ukwaju
(III) B29(sabuni ya kipande)- Mo29
(IV) Azam cola- Mo cola
(V) Kleesoft(wachina)- Clean soft. Dadeq hapa akaingia choo cha kike kawakopi wakongwe wa kukopi na vile mwizi akiibiwa anavoumia vijamaa vikampeleka tume ya ushindani na biashara.
Kesi ikasikilizwa ikaonekana Tz's top copycat aka bilionea mwenye ubahili wa kijasiriamali aliiga kuanzia jina linavosound, rangi ya bidhaa na kifungashio. Kama kawaida za mwizi arobaini sabuni yake ikapigwa pini na haitakiwi kuonekana sokoni labda watumie washabiki wa mikia fc kufulia yale madaso yao mekundu wakiwa magetoni.

NB
Uzi hauhusiani kwa vyovyote na wala usihusishwe na upinzani wa jadi uliopo kati wapenzi na washabiki wa timu ya Wananchi dhidi ya waturutumbi na wasukutua mdomo kwa viroba wa mikia fc.

Naomba kuwakilisha na povu ruksa
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€

Sasa Azam wametangaza kuwa wapo mbioni kutoa Ubuyu Icelolly...kazi ipo kwa photocopy machine sasa.

Imekopi Boko, Manula, Nyoni, Wawa 😷
 
Huyu asije kujichanganya akaja na moboeing au iPhomo, wamarekani watampiga wamchakazeπŸ˜€πŸ˜†
 
😝😝😝😝Mkuu umesema uzi hauhusiani na upinzani wa jadi, lakini mwisho umewapa madogo,
Watawezaje kuvumiliaaa?πŸ˜‚πŸ˜‚
Wakishindwa kuvumilia nimewaruhusu kutoa povuπŸ˜€πŸ˜†πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…