Best place to stay in Kigoma/ Sehemu nzuri za kufikia

R579

Member
Joined
Dec 22, 2023
Posts
92
Reaction score
110
Nategemea kutembelea mji wa Kigoma mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu. Kwa mwenye uzoefu na mji wa Kigoma, naomba kufahamishwa sehemu nzuri ya kufikia na maeneo ya kutembelea kwa wiki tatu nitakazo kaa kule.

Naenda kupumzika likizo.
 
Unaweza kufikia Mwitongo, Malagalasi, Lake Tanganyika, Hill top, Aqua etc. Kuna hoteli na lodges nzuri ni pesa yako tu.

Sehemu za kutembelea unaweza kwenda

1. Gombe
2. Mahale
3. Dr. David Livingston makumbusho
4. Mwisho wa reli (ulipoishia reli)
5. Manyovu mpakani mwa Tanzania na Burundi
6. Kibirizi ukajionee soko la dagaa kigoma
7. Ujiji mji mkongwe wa Kigoma
8. Kagera Ujiji ukajionee miti ya maembe yalivyojipanga ambayo yalipandwa na watumwa wakati wakisafirishwa kuelekea Bagamoyo
9. Beach mbalimbali za mkoa wa Kigoma
 
Asante sana kwa taarifa hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…