Best yangu akimbizwa na vibwengo kwa miguu kutoka Mbande Mbagala mpaka Kariakoo sokoni

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Wakuu,

Kuna best yangu moja anaishi Mbande Mbagala majuzi mida ya saa 8 usiku kakimbia kwa miguu kutoka mbagala mpaka Kariakoo sokoni. Picha kamili ilikua hivi:

Huyu best yangu anakata sana maji, sasa majuzi alitoka pale Dar live akiwa kalewa sana mida ya saa nane usiku na kuelekea kwake alipofika mbande akachepuka kidogo kichakani kujisaidia haja ndogo.

Sasa alipokua akijisaidia mara akavikojolea vibwengo vilivyokua vimelala pale kichakani mara vikakurupuka kama vimefumaniwa vile mazee vijomba vimejazia kama Pawa Mabula vinamsuli hatari halafu vifupi kama stuli,jamaa alivyoona akapata shock na kutimua mbio kama usein bolt navyo vilivyoona jamaa anatimua vumbi halafu kavilowanisha vikaamua kumuunganishia marathon.

Jamaa alikimbia sana kurudi Dar live kwa miguu mara alipofika akakuta wamefunga mageti na vibwengo vinampumulia kisogoni dah! Jamaa akakamua tena mbio mara kuja kushtuka yuko sokoni Kariakoo.

Chezea vibwengo wewe. Jamaa ameacha kunywa pombe
 
Umeharibu sehemu moja tu stori ingeaminika.

Distance kutoka mbagala mbande hadi kariakoo si mchezo .

Tunashukuru kwa soga hii.
 
Angewangoja awape Hi tu. Story mbili tatu nn. Kujishtukia kwake.
 
Wakuu,

Kuna best yangu moja anaishi Mbande Mbagala majuzi mida ya saa 8 usiku kakimbia kwa miguu kutoka mbagala mpaka Kariakoo sokoni. Picha kamili ilikua hivi:

Huyu best yangu anakata sana maji, sasa majuzi alitoka pale Dar live akiwa kalewa sana mida ya saa nane usiku na kuelekea kwake alipofika mbande akachepuka kidogo kichakani kujisaidia haja ndogo.

Sasa alipokua akijisaidia mara akavikojolea vibwengo vilivyokua vimelala pale kichakani mara vikakurupuka kama vimefumaniwa vile mazee vijomba vimejazia kama Pawa Mabula vinamsuli hatari halafu vifupi kama stuli,jamaa alivyoona akapata shock na kutimua mbio kama usein bolt navyo vilivyoona jamaa anatimua vumbi halafu kavilowanisha vikaamua kumuunganishia marathon.

Jamaa alikimbia sana kurudi Dar live kwa miguu mara alipofika akakuta wamefunga mageti na vibwengo vinampumulia kisogoni dah! Jamaa akakamua tena mbio mara kuja kushtuka yuko sokoni Kariakoo.

Chezea vibwengo wewe. Jamaa ameacha kunywa pombe
Watu wa Mbagala wakishashiba hawakosi cha kusimulia
 
Back
Top Bottom