Kwani kuna kosa kama nta deposit bila pesa kuchezea kamari kwa siku kadhaa kisha nikaitoa pesa yangu? embu nipe kifungu kinachosema nikosa kisheria nijifunze hapa
Utakuwa Unakutwa na Makosa kama Sita hivi 🤣
Kosa la Kwanza
Money Laundering, Kosa la Pili
Misuse of Financial Sevices, Kosa la Tatu
Evasion of Reporting Obligation na
Tax Evasion...
Japo Kuna makosa Kama
Money Laundering Unaweza Ukaliepuka kama
Financial Intelligence Unit(FIU) wakithibitisha Hizo pesa Umezipata Kihalali na wakawa na Uhakika wa Halali yako na Uchunguzi ukafanyika Ikagundulika Kweli pesa Ulizipata Kihalali ila zisiwe na makando kando na ukaziweka kwenye wallet ya Bet Apps...
Ila hayo makosa Mengine Hukwepi Bablai Hiyo Debe inakuhusu..
Ngoja Nikuchambulie sasa..
1.Money Laundering (Sheria ya Anti-Money Laundering Act, 2006)
Under Section ya 12 ya Anti-Money Laundering Act, 2006, Utakuwa Umefanya Kitu kinaitwa..
Prohibited Activities:
Nanukuu Sheria
“A person commits the offense of money laundering if they directly or indirectly conceal, disguise, convert, transfer, or handle funds they know or ought to know are proceeds of unlawful activities.”
Penalty:
“Any person who commits the offense of money laundering shall, on conviction, be liable to a fine of not less than TZS 500 million or to imprisonment for a term of not less than seven years and not more than ten years, or both.”
Kwenye scenario yako ya Kuweka pesa kwenye betting wallets na Ku withdraw money without engaging in betting, this may be viewed as a way to obscure the origin of the funds (a key indicator of money laundering).
Na ndo maan nimesema Hapo FIU (Financil Intelligemce Unit) watafanya Uchunguzi Kama Ni kijana Tu huna Kazi ya halali ya Kufanya (Umeishaaa) kama Pesa Uliyoweka Ni Zaidi ya Mshahra wako au 60% ya Mshahara wako Itabdii Utoe Maelezo ya Kutosha Pesa Umetoa wapi na Kuziweka kwenye apps wallet ukiwa Huna maelezo ya Kutosha Hili kosa Linakuhusu..
2. Misuse of Financial Services (The Banking and Financial Institutions Act, 2006)
Kwa kutumia Section ya 17 ya Banking and Financial Institutions Act, misuse of financial services iko prohibited..
Nanukuuu:
"No person shall use a financial institution, e-money wallet, or other regulated service in a manner inconsistent with the purposes for which the service is designed."
Penalty:
“A person who contravenes this provision commits an offense and is liable to a fine or such administrative penalties as prescribed by the Bank of Tanzania.”
Sasa kwenye Hili Kosa Huchomoki Hata Ukichomoka kwemye Utakatishaji pesa Ila kwenye Hili Mzee Hutoki kwa sababu umetumia Application kama Benki wakati sio matumizi yake kile kitendo cha kutumia betting wallets as a “bank” without participating in the intended activities yaani betting constitutes misuse of the platform na Hapa wanaweza kukusamehe wakakuchapa Penalty tu ila Kifungo hapa Hakuna.na inategemea na Huruma ya BOT
ila Mimi nina uhakika Lazima wakudake na Yote..
maana Kuthbitisha Pesa ya Halali kwa Tanzania Ni Changamoto kidogo..
3. Evasion of Reporting Obligations (Anti-Money Laundering Act, Section 17)
Sasa hapa kama wakikukuta na Makosa Hapo juu yote mawili hapaa lazima waangalue kama Pesa uliyo deposits au withdrawals exceed the reporting threshold (e.g., TZS 10 million for suspicious transactions) and the user intentionally structures transactions to avoid reporting:
Nanukuu:
"
Any person who structures transactions to avoid statutory reporting requirements commits an offense.”
Penalty:
“A fine not exceeding TZS 100 million or imprisonment for a term not exceeding five years, or both.”
4. Tax Evasion (Income Tax Act, 2004)
Ikitokea Umewashinda kwenye Money Laundering Mama Yangu Hiyo ya Pili na ya tatu Huchomoki ila Ukichomoka Ukatoa na Ushahidi Kuwa Hizo pesa Ni za kwako na Umetoa kwenye Biashara yako au Kazi yoyote nyingine na Hicho kiwango ulichokitoa Ukadeposit kwenye Wallet apps hujareport TRA au hakijawa declared to the Tanzania Revenue Authority (TRA) mamamaaamaaaaa Imba Ile Nyimbo Ya Kasongo ti 😅😅🙌🙌
NAnukuu:
“Any person who fails to report taxable income or engages in transactions intended to obscure income commits the offense of tax evasion.”
Penalty:
“A fine equal to twice the tax amount evaded, or imprisonment for a term not exceeding three years.”.
nafikiri Mpaka Hapo Umenielewa..
Na Kumbuka Kutokujua Sheria Sio Excuse ya Kuvunja Sheria 😅😅
Nakutakia Kazi njema Ya Kudeposit Pesa kwenye Application za Betting na Kuzitoa Baada ya Siku kadhaa huku Ukisubiri wakudake ili Wakuonyshe sehemu salama ya Kutunza Pesa