Beware usije ukatapeliwa. Big_Sales is a con man.

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,637
Reaction score
47,413
Najua pesa imekuwa ngumu sana mtaani. Inapatikana kwa shida sana, so chunga usije kuitoa kwa urahisi.

Kuna jamaa mmoja huko IG anajiita "big sales" akijinadi kuwa ni official samsung na LG seller kwa east africa. Ukitembelea page yake anavitu vingi vizuri, ila vinapatikana kwa bei chee sana. Location yake anasema ni Chakechake Pemba, opposite na NMB bank ya zamani.

Wandugu huyo mtu ni tapeli na hana duka kule Pemba. Mpaka sasa najua wengi sana wameshalizwa na huyu jamaa, ila wanalia kimya kimya.

Najua JF sio mahala pake, ila nimeamua kuandika hapa nikiamini wengi wapo humu. Na sababu ya kuandika imetokana na kukutana na binti ambae alikuwa amekubalia na big sales amuuzie Iphone kwa tsh milion moja. Binti katanguliza laki 7,hiyo 3 iliyobaki wakakubaliana ataimalizia akishapatiwa mzigo wake. Baada ya kulipa, binti alifika hadi pale dukani akagandishwa zaidi ya masaa 4 anasubiria. Baadae ikabidi akubali kuwa kalizwa, akaondoka analia.

Sababu ya pili ambayo pia imepeleka niandike ni kumsaidia yule Mzee halisi mwenye duka lililopo opposite na NMB bank pale chake. Huyu Mzee ameshapata kesi na malalamiko mengi ambayo hayajui, imefikia hatua ameenda polisi kulipoti na kupatiwa RB. Maana wateja wanaenda pale kwa wingi kufata mali zao walizolipia ambazo yeye (Mzee) hazifahamu.



Hapo juu ni link ya ukurasa wa wa huyo mtu anayejiita big sales.

To share is to care.

Thanks.

Analyse.
 
Mjini akili nguvu kijijini muache ajipigie pesa.
 
Huyu alikuwa na bei ambazo, haziwekani katika usawa huu... Kuna mtu alitaka kumtumia hela, akampigia kumcheki, kwenye true caller ikaonyesha jina TAPELI, ndio ilikuwa salama yake.. Umefanya vizuri kuleta huu uzi, utaokoa wengi...
 
Ahsante kwa taarifa,


Lakini Watanzania na sisi tumezidi, ni kama akili zetu hazikuanikwa juani zikakauka vizuri hivyo kubaki zimevunda.
 
me wauzaji wa online wa kitanzania sijawahi kuwaamini. tukikubaliana ni lazima tuonane tukabidhiane, mambo ya kutuma pesa eti mzigo nitatumiwa huwa sifanyi uzembe huo.
 
Huyu alikuwa na bei ambazo, haziwekani katika usawa huu... Kuna mtu alitaka kumtumia hela, akampigia kumcheki, kwenye true caller ikaonyesha jina TAPELI, ndio ilikuwa salama yake.. Umefanya vizuri kuleta huu uzi, utaokoa wengi...
Hahahaha shkamoo true caller
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…